TUKIO LA NAIBU WAZIRI MTEULE KUSHINDWA KUAPA,LAACHA MASWALI

 

Ilikuwa furaha kwa Mawaziri na Manaibu wao kuwasili Ikulu jijini Dodoma na kula viapo vyao vya uaminifu mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Magufuli.

Tukio hili lilikuwa likifuatiliwa moja kwa moja kupitia runinga mbalimbali zilizokuwa zinarusha mubashara kutoka eneo la tukio-Chamwino   Jijini  Dodoma.

 Tukio lililoacha maswali kwa wengi lile la Naibu Waziri wa Madini, Ndulane Francis Kumba kushindwa kuapa hivyo kufanya manaibu Waziri walioapa kuwa 22 kati ya 23 walioteuliwa..Kutoka na kitendo hicho cha mteule huyo kushindwa kusoma kiapo chake,Rais Dkt. John Magufuli amesema nafasi hiyo atateuliwa mtu mwingine mwenye uwezo wa kuapa na kusimamia kazi.

Tutatafuta mtu mwingine atakayeweza kuapa vizuri,kusoma vizuri ambaye akipelekwa kwenye madini ataweza kusoma document(nyaraka) vizuri ili zisije zikawa fojidi (batili),huo ndio ukweli.

Dkt.John Magufuli.

 Ndulane Kumba ambaye ni Mbunge  Kilwa Kaskazini aliondolewa mbele ya Rais Magufuli na viongozi mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo baada ya kushindwa kusoma vyema maneno ya kiapo hicho.

 

 


Post a Comment

0 Comments