(TFS) WALIVYOSHIRIKIANA NA JESHI KUPANDA MITI.

 


📌Na DEVOTHA SONGORWA.

WAKALA wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) wakishirikiana na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wamesheherekea Maadhimisho ya miaka 59 ya Uhuru kwa kupanda miti katika hospitali ya Uhuru iliyopo Chamwino.

 Akizungumza na waandishi wa habari Meneja wa Wakala huo  Kanda ya Kati Mathew Kiondo amesema  hatua hiyo ni kuenzi mema yaliyofanywa Hayati Rais Julius Nyerere na wapigania Uhuru wa Tanganyika Disemba 9,1961.

 Amesema kujengwa kwa hospitali hiyo na kupewa Jina la Uhuru inaonyesha maana halisi ya uhuru hivyo itakuwa msaada mkubwa kwa taifa akisema kwamba upandaji wa miti ni kuhakikisha watanzania wanaishi katika mazingira salama.

 "Tumeungana na wenzetu wa JKT kupanda miti na tumetoa miti 4000 katika bustani zetu na tupongeze kwa uamuzi huu hospitali Ni kubwa na ya kisasa tunatamani kila Wilaya ingekuwa na Hosptali ya kiwango hiki",alisema Meneja huyo.

 Akizungumzia uhifadhi wa misitu aliwataka wananchi kuzingatia Sheria zilizopo katika uchomaji mkaa na kuepuka kukata miti ovyo inayosababisha ukame,mabadiliko ya tabia nchi na kukosa hewa safi.

 "Yapo mafanikio makubwa katika sekta hii kabla ya uhuru na baada ya uhuru  hata idadi ya misitu imeongezeka,tuna mashamba zaidi ya 20 ya misitu, tuna vitendea kazi vya kisasa kwa kweli tunawapongeza waasisi wetu na usimamizi wa misitu umebadilika tunasimamia kama Jeshi la Uhifadhi Tanzania kukabili uharibifu wa misitu yetu.

 Nishati ya mkaa ni muhimu sana majumbani lakini hatuta mhurumia atakayekiuka sheria za misitu za uvunaji wa maka  kwa sababu kwani  inatakiwa kila Wilaya kutenga eneo kwa kazi hiyo na tuna utaratibu mfanyabiashara awe na leseni,ulipe ofsi kodi na kuonyeshwa eneo husika na kukata miti kwa ajili ya kuchoma mkaa",alisisitiza Kiondo. 

 Kwa upande wake Kanali Hassan Mabena Kaimu Mkuu wa Utawala Jeshi la Kujenga Taifa(JKT) alieleza kwamba hosptali hiyo ilianza kujengwa tangu maadhimisho ya Uhuru mwaka 2018 na hadi sasa imefikia asilimia 97% kw pamoja na miudo mbinu yake na kufikia Disemba 15 itakuwa imekamilika.

 “Fedha zilizokuwa zitumike kwa sherehe zimeletwa huku kukamilisha ujenzi na vitu vyote vinavyohitajika inaze kazi haraka  kuondoka changamoto ya wananchi kutembea umbali mrefu kutafuta huduma na jeshi tumepewa kazi ya kujenga tukipata ushauri wa TBA na hamshauri ya chamwino kuhakikisha mani iliyopo na uhuru tunavilinda",alisema Mabena.

 Katika hatua nyingne Luteni Kanali Mkuu wa Kambi Makao Makuu (JKT) alibanisha kwamba mbali na kupanda miti 400 wamefanya usafi katika zahanati ya Chamwino akisema kwamba wanatarajia mabadiliko makubwa  kwa nyanja ya mazingira.

 Aidha Mwenyekiti wa Baraza la Wazee  CCM Dodoma mjini na Meya mstaafu wa iliyowahi kuwa Manispaa ya Dodoma,Peter Mavunde alieleza mabadiliko makubwa yaliyofanywa katika harakati z akupoigania uhuru akielelza kwamab uhuru huo umeletema mabadiliko ya kihoistori na kutembea katika mnyororo wa kuondoa ujinga, umasikini na maradhi.

 " Mwalimu Nyerere  alitangaza vita dhidi kuondoa, umaskini na maradhi pia alijenga chuo kikuu kimoja na zile shule za sekondari zingnez zilikuwa za dini alitaifisha na wanafunzi wote kusoma kwa pamoja, alianzisha elimu ya watu wazima hata leo Rais Magufuli anatembea nyao zake tujivunie viongozi wetu",alisema Mavunde.

 Kaulimbiu ya mwaka huu ni Miaka 59 Uhuru na miaka 58 ya Jamhuri Tanzania yenye Uchumi Imara Utajengwa na watanzania wenyewe ,tufanye  kazi kwa bidii, uwajibikaji na uadilifu.

Post a Comment

0 Comments