📌FAUSTINE GIMU .
MAMLAKA ya Usimamizi wa Wanyamapori nchini (TAWA)imezindua Duka la kwanza hapa nchini litakalokuwa likijihusisha na
uuzaji wa nyama zitokanazo na wanyamapori
.
Akizungumza katika uzinduzi wa duka hilo la Wanyamapori Disemba 20,2020 katika mtaa Kishoka kata ya Chang’ombe
jijini Dodoma,Mwenyekiti wa Bodi Mamlaka
ya Usimamizi wa Wanyamapori(TAWA)Meja Jenerali Mstaafu Khamis Semfuko amesema lengo la kufungua duka
hilo la wanyamapori ni katika kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli katika kuhakikisha Watanzania wananufaika
na rasilimali za Tanzania.
Lazima tuanzishe Maduka ya kuuza wanyamapori katika maeneo mengi na hapa nimekuja kufungua duka letu la kwanza la uuzaji wa wanyamapori ili kutekeleza amri hiyo ya Amiri Jeshi wetu.
Meja Jen (Mstaafu) Semfuko
Aidha,Jenerali Semfuko amebainisha kuwa wanyamapori watapatikana kwa njia ya vibali
maalum ya uwindaji,kwa wawindaji wa kitalii,na kwa wananchi wenyewe
watakaoanzisha Lanchi za kufuga wanyamapori ambapo ameahidi kuwa TAWA ipo tayari kuwapatia
Mitamba ya uanzishaji ufugaji wanyamapori.
Pia,amebainisha kuwa Mabucha ya wanyamapori
yatapatikana katika maeneo mbalimbali nchini huku ujangili wa wanyama
utaendelea kuthibitiwa na usafi
utazingatiwa na utaratibu wa uanzishaji wa mabucha ya wanyamapori upo
wazi .
Wadau wa biashara ya nyamapori wakiwa katika picha ya pamoja na maafisa wa TAWA mara baada ya uzinduzi wa duka la nyama pori jijini Dodoma |
Kaimu Kamishna wa Uhifadhi kutoka Mamlaka ya
Usimamizi wa wanyamapori Tanzania(TAWA)Mabula Misungwi Nyanda amesema
Bucha la nyama za Wanyamapori lililozinduliwa limetokana na
wanyama waliowindwa huku akitoa wito
kuwa ukitaka kula nyamapori lazima uijue TAWA kwani ni Msimamizi mkuu wa
wanyamapori katika masuala ya uvunaji.
Wananchi wa Mtaa
Kishoka Mtaa kata ya Chang’ombe jijini Dodoma akiwemo Mwenyekiti wa mtaa
huo Juma Maulid,na Mariam Juma Damas wameelezea kufurahishwa kwao kuanzishwa
kwa bucha la nyamapori kwani itawarahisishia kupata nyama kiurahisi.
0 Comments