📌Na RAMADHAN HASSAN
WAZIRI
wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Profesa Joyce Ndalichako ameshangazwa na
Maafisa elimu kutoa takwimu za wanafunzi wa kike ndio wanaongoza
kwa kuacha masomo kutokana na kupewa mimba wakati takwimu alizonazo
wanafunzi wa kiume ndio wanaongoza kwa kuacha masomo na kwenda kufanya
biashara.
Pia,amewataka
Maafisa hao kusimamia ubora wa elimu unaotolewa katika maeneo yao ikiwa
ni pamoja na kuhakikisha Maafisa elimu wa taaluma,michezo,utamaduni,elimu
maalum na takwimu wanatimiza wajibu wao.
Kauli
hiyo ameitoa leo wakati akifungua mkutano wa saba wa Chama cha Maafisa Elimu wa
Mikoa na Wilaya (REDEOA).
Profesa
Ndalichako amesema takwimu ambazo anazo zinaonesha kwamba wanafunzi wa kiume
wengi ndio wanaoacha masomo na kwenda kufanya biashara lakini kila siku
Maafisa elimu wamekuwa wakitoa takwimu za mimba za wanafunzi wa
kike kupewa mimba.
“Naomba
tuwaheshimu watoto wa kike baadhi ya kauli zinazotolewa zinakuwa hazina afya na
zinakuwa ni za udhalilishaji kwani ni watoto wetu hata wale wanaopata ujauzito
tuwaone kama binadamu kwa sababu wakati mwingine kauli zinazotolewa hazipendezi
na niwaombe Maafisa elimu, kuna takwimu za kutoa kila siku mimba tu inakuwa
kama vile hakuna kitu.
“Takwimu
zangu zinanionesha watoto wa kiume ndio wengi wanaoacha masomo na takwimu
hizi zinatoka kwenu sasa kama zimechakachuliwa mmezileta nyinyi hasa katika
maeneo ambayo ni ya wavuvi na wafugaji unaona saa za shule wanauza kwenye
mabasi wale kwani hamuwaoni?.
“Naomba
tusimamie elimu yetu tunaposimamia watoto wanaocha shule tuangalie makundi yote
na kutafuta sababu kama suala la mimba tunaendelea kujenga mabweni. Naomba sana
unakuta takwimu ni mimba tu kama vile hakuna kitu kingine hiyo single yenu ya mambo
ya mimba tumeichoka hii awamu ya tano mje na single nyingine.kila siku wimbo
mmoja Serikali ya Magufuli ipo imara,”amesema.
Prof.Ndalichako
amesema sekta ya elimu inafanya kazi vizuri lakini yeye anataka wafanye vizuri
zaidi ikiwa ni pamoja kuwasimamia Maafisa elimu wote waliopo katika maeneo yao
kuhakikisha wanatenda kazi ambayo wanatakiwa kuifanya.
“Tunafanya
vizuri lakini tunataka tufanye vizuri zaidi kwahiyo kila mmoja akawajibike.
Nataka mkaweke mfumo thabiti wa kuwasimamia, waweze kuwajibika,Afisa elimu
utamaduni akawajibike afisa elimu taaluma akawajibike,takwimu akawajibike,
nadhani katika sekta ambayo imepewa watumishi wengi ni pamoja na sekta ya
elimu.
Vilevile,Waziri
Ndalichako amesema Serikali imejipanga kuhakikisha inazidi kuboresha masomo
yote yanawajengea uwezo wanafunzi kwenye maisha yao ya kawaida kama
masomo ya kilimo.
“Tutahakikisha
tunaendelea na masomo ya michepuo kwa sababu wakimaliza tayari wanakuwa fmafundi
na wataalamu wa kushona nguo awe na utaalamu wa kilimo naamini tutayatekeleza
uchaguzi umeisha sasa ni kuchapa kazi,”amesema.
Hata
hivyo,amewatoa hofu Maafisa Elimu Wilaya kwa kudai kwamba Serikali imeishaagiza
magari 184 kwa ajili yao ambapo mpaka ifikapo Januari 15 mwaka huu yanatakuwa
yameishafika nchini.
“Serikali
hii haina ahadi hewa nawaomba wanaohusika na manunuzi wanapoanza mwaka Maafisa
elimu wawe na magari yao kuweza kufika maeneo mbalimbali,”amesema
Prof.Ndalichako.
Aidha,Waziri
Ndalichako amewataka Maafisa elimu hao kusimamia elimu maalum kwani ni kundi
ambalo linahitaji kusaidiwa kwani kundi hilo ni wachache.
“Jambo
lingine nawaomba tusimamie elimu maalum na ninaomba mjitume zaidi kwani
bado kuna chagamoto zipo kuna baadhi ya Wilaya zinafanya vizuri na
zingine zinafanya vibaya wale wenye mahitaji maalum wanatakiwa kuangaliwa kwa
jicho la kipekee.Ni jukumu la Serikali kuwasaidia na watu wenye ulemavu
tunawapa mikopo kwa asilimia 100.
Amesema
Serikali ipo katika mpango wa kujenga shule ya wanafunzi wenye mahitaji maalum
ya Viziwi katika eneo la Lukuledi Mkoani Mtwara.
Katika
hatua nyingine,Waziri Ndalichako amesema Serikali imefanikiwa kupata mkopo wa
shilingi trilioni 1.2 kutoka Benk ya dunia ambazo zitatumika kujenga shule mpya
za sekondari 1000 pamoja na shule za kidato cha tano na sita 26 kwa ajili ya
maso
0 Comments