📌NA SALEH RAMADHANI.
IMEELEZWA kuwa taarifa sahihi za hali ya hewa zikiwafikia
wachimbaji wa madini kwa wakati,zitaisaidia kukabiliana na changamotoza
mabadiliko ya hali ya hewa.
Hayo yamesemwa na Mhandisi Aron Kisaka wakati akimwakilisha
katibu mkuu wa sekta ya uchukuzi katika ufunguzi wa mkutano wa wadau wa sekta
ya madini unaojadili umuhimu wa huduma
za hali ya hewa.
Amesema kuwa taarifa hizo zitazisaidia mamlaka zinazohusika
kupanga mipango ya kukabiliana na majanga ndani ya sekta yatokanayo na hali
mbaya yahewa kama maporomoko ya udongo.
“Katika mkutano huu washiriki watapata fursa ya kufahamu faida
za utumiaji wa taarifa za hali ya hewa kwa sekta ya madini”amesema.
Aeongeza kuwa matumizi ya huduma za hali ya hewa yanatarajiwa
kuongeza tija,ufanisi na usalama katika shughuli zinazohusianana
utafutaji,uchimbaji madini na uendeshaji wa migodi.
Awali Mkurugenzi Mkuu wa
Mamlaka ya Hali ya hewa Tanzania (TMA) Dk. Agnes Kijazi amesema,mamlaka ya hali
ya hewa inatoa huduma mahususi kwaajili ya sekta mbalimbali nchini ikiwemo ya
madini.
Amesema kuwa pamoja na elimu hiyo bado wadau wa sekta ya madini
wahazitumii ipasavyo huduma hizo.
“Ni matarajio yetu kuwa wadau watapatiwa elimu ya matumizi
sahihi ya huduma za hali ya hewa na huduma zitakazo patikana endapo watazitumia
vyema taarifa hizo”amesema Kijazi.
Naye Mwakilishi wa Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa mamlaka
ya hali ya hewa Tanzania Robert Sunday amesema madhumuni ya mkutano wa sekta ya
madini na mamlaka ya hali ya hewa ni kuunganisha nguvu katika kuhakikisha
kunaongeza pato la taifa na usalama wa watu na mali zao.
Mwisho.
0 Comments