SPIKA NDUGAI AWAAHIDI MEMA WATU WENYE WALEMAVU

 


 ðŸ“Œ HAMIDA RAMADHANI

SPIKA wa Bunge Job Ndugai amesema Bunge litahakikisha wanaondoa vikwazo kwa Watu wenyewe ulemavu  kwa kuweka mazingira rafiki kwenye mikopo kwani mazingira yaliyowekwa kwa makundi ya watu wenye ulemavu kwa ajili ya kupata mikopo ya halmashauri siyo rafiki kwao  

Pia amehimiza ujenzi wa miundombinu rafiki kwenye taasisi za Serikali inayozingatia watu wenye ulemavu . 

Spika Ndugai ameyasema hayo wilayani Kongwa katika mkoa wa Dodoma wakati wa maadhimisho ya watu wenye ulemavu ambayo hufanyika Disemba 3,kila mwaka yenye lengo la kuelimisha jamii kuhusu haki za watu wenye ulemavu katika kujua mahitaji yao,changamoto zao na namna ya kuzitatua.

Amesema,licha ya kuwa nao wanatambulika katika kupatiwa mikopo lakini wamekuwa na  masharti magumu likiwemo la kuwataka wajiunge katika vikundi vya watu watano .

Neno vikundi linaleta matatizo makubwa na kupelekea wengine kushindwa kupata mikopo kutokana na masharti yaliyowekwa.

Spika Ndugai

 Amesema mikopo inapaswa itolewe kwa ngazi ya familia ,mtu mmoja mmoja kulingana na hitaji la mtu husika.

"Haiwezekani watu wenye ulemavu kulazimishwa kuwa katika makundi wakati unakuta katika sehemu moja labda kuna walemavu wawili,sasa kikunsi kinataka watu watano,hao wengine wanapatikana wapi,suala hili inabidi ulitazame upya." Amesema na kuongeza kuwa

Nakubaliana nanyi kwamba masharti siyo rafiki,ila walengwa wanapochukua mikopo hii wahakikishe  wanairudisha ili na wengine waweze kupata fursa hiyo.


Aidha Spika Ndugai amesema atawapa ushiriliano wavunge wanaowakilisha watu wenye ulmavu ili kufanya maisha yao yawe bora zaidi ifikapo mwaka 2025.

Awali  Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la watu wenye ulemavu nchini (SHIVYAWATA) Tungi Mwanjala ameiomba Serikali kutoa bure vifaa vya watu wenye ulemavu kutokana na vifaa hivyo kuuzwa bei ghali na hivyo wengi kushindwa kumudu gharama hizo.

 Pia alitaja changamoto zinazowakabili ni pamoja na kutokiwa na miundombinu rafiki hasa katika majengo ya serikali,upatikanaji wa matibabu ,ukosefu wa ofisi kwa wenye ulemavu,kutokiwepo kwa bajeti ya kutosha kwa watu wenye ulemavu na kuwapatia bima ya afya.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Dodoma ,Mkuu wa wilaya ya Kongwa Dkt.Suleiman Selela amesema ,maadhimisho ya mwaka huu yamelenga kuifikia jamii hasa ya vijijini kutokana na maadhimisho hayo kufanyika wilayani.

Amesema licha ya Serikali kuzifanyia kazi changamoto za wenye ulemavu,lakini bado kuna changamoto ambazo mkoa unazifanyia kazi katika kuzitatua.

Post a Comment

0 Comments