📌Stephen Noel-Mpwapwa
MKUU wa Tasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa(TAKUKURU) wilaya ya Mpwapwa bi: Julieth Mtuy amewataka Madiwani wapya kuhakikisha wanasimamia miradi ya Maendeleo kwenye Kata zao ili kuweza kuharakisha Maendeleo ya Mpwapwa.
Bi Mtuy ameyasema hayo alipokuwa akiwasilisha mada kwenye kikao cha Madiwani Jana ya athari za Rushwa katika Maendeleo.
"Msimamie mapato yanayotokana na miradi iliyopo katika maeneo yenu, Kama vile miradi ya maji ili fedha zinazopatikana zilete tija na kuwainua wananchi kiuchumi"ameongea.
Aidha amesema kuwa kwa sasa madiwani hao wameaminiwa na wananchi pamoja na chama hivyo wanawajibu wa kutimiza majukumu yao kwa kuzingatia sheria kanuni na maadili ya uongozi wao.
Pia ameongeza kuwa Ofisi yake haitavumilia vitendo vyote vya vinavyo ashiria rushwa katika miradi na pesa za umma.
Mmoja wa wananchi wa wilaya ya Mpwapwa, Emanuel Ndule amesema rushwa imekuwa changamoto katika miradi mingi ya Maendeleo katika wilaya ya Mpwapwa na kuisababisha wilaya hiyo kushindwa kupiga hatua za maendeleo kwa wakati.
Mwisho.
0 Comments