Shule za Msingi zatakiwa kuchangamkia Fursa za Miche.

 



Na RAMADHAN HASSAN

SHULE za Msingi Jijini hapa zimetakiwa kuchangamkia fursa ya kupata miche 100 ya miti ya vivuli na matunda  kutoka katika Kikundi cha uhifadhi na utunzaji mazingira cha Chapakazi kwa sharti la kuhakikisha inaota na haifi ili kutunza mazingira.

Hatua hiyo imekuja kufuatia kikundi cha Chapakazi hivi karibuni kutangaza kutoa miche 100 kwa kila shule ya msingi katika Jiji la Dodoma kwa lengo la kutunza mazingira.


Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Desemba 7 mwaka huu Jijini hapa,Mtunza fedha wa kikundi hicho,Darwesh Said amesema wameamua kutoa miche 100 ya miti ya vivuli na matunda kwa shule zote za Jiji la Dodoma kwa lengo la kutunza mazingira.

Darwesh amesema utunzaji wa mazingira ni muhimu hivyo jamii inatakiwa kupanda miti kwa wingi husasani katika kipindi hichi cha mvua .

Amesema kutokana na umuhimu huo,Kikundi cha Chapakazi kimeamua kutoa miche 100 kwa shulke za msingi  ili kutunza mazingira ya Jiji la Dodoma.

“Tunatoa miche 100 kwa kila shule za Jiji la Dodoma lengo letu ni kutunza mazingira na kuifanya Dodoma kuwa ya kijani,sisi kikundi cha Chapakazi hii ndio dhamira yetu na tumeendelea kuhakikisha mazingira ya Jiji la Dodoma yanakuwa katika ubora,”amesema.


Post a Comment

0 Comments