Balozi
wa Ufaransa Nchini Tanzania ,Frederic Clavier ameyasema hayo jijini Dodoma mara baada ya kufanya
mazungumzo na Katibu Mkuu wa CCM Dk Bashiru Ally.
Bila
kufafanua zaidi kuhusu idadi ya fedha na wanufaika, Clavier amesema
amefurahishwa na Serikali ya CCM juu ya mipango ya kuwawezesha vijana na kuwapa kipaumbele katika fursa za
maendeleo.
“Tumekutana
tujadili mambo muhimu kuona mwenendo wa Taifa hili hususan baada ya kushiriki
uchaguzi mkuu. Lengo ni kuboresha
mahusiano mema kati ya nchi hizi mbili kwa muktadha huo nchi yangu itasaidia mafunzo ya ufundi kwa
vijana kwa asilimia 100 ili kuleta maendeleo,”amesema.
“Ninapongeza hotuba ya Rais John Magufuli
wakati wa uzinduzi wa Bunge jijini Dodoma kuhusiana na sekta binafsi. Sasa
uchaguzi umepita ni wakati wa kurudi na kufanya kazi ya kulijenga Taifa kwa
manufaa ya wananchi,”amesema
Pamoja
na hayo,Cleaver ameambatanisha pongezi
hizo na ujumbe maalum wa barua kutoka nchini ufaransa wenye lengo la kupongeza
juhudi za rais wa Tanzania dkt.John Magufuli.
Kwa
upande wake katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dk Bashiru Ally amesema mipango
waliojadili imelenga kuinua maendeleo ya vijana wa Tanzania katika maeneo ya
vyuo ufundi ambayo yatakuza ujuzi na maarifa hasa kwenye uzalishaji.
0 Comments