SAKATA LA KUUNGUA KWA MABWENI ,SULUHISHO LAPATIKANA.

 



📌HAPPNESS MTWEVE.

 KUTOKANA na uwepo wa matukio ya kuungua kwa mabweni ya shule za Sekondari Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini kwa kushirikiana na Chama cha Skauti Tanzania wameingia mkataba wa makubaliano wa kutoa elimu ya kukabiliana na majanga ya moto yanayosababishwa na hitilafu mbalimbali za dharura

Skauti mkuu wa Tanzania Mwantumu Mahiza akizungumza wakati wa kusaini makubaliano hayo amesema vijana wa skauti wamekuwa wakishiriki katika matukio mbalimbali ya uokozi ikiwemo majanga ya moto yanayotokewa hapa nchini.

Mahiza amesema kupitia makubaliano hayo watahakikisha wanatoa elimu ya kukabiliana na majanga mbalimbali kwa kushirikiana na jeshi hilo.

Amefananua kuwa  makubaliano hayo yanataraji kuanza mapema Januari mwakani, utasaidia kufanya kazi kwa pamoja na kufahamu na kufanikisha masuala ya uokozi kwa urahisi nchini.

Kamishna wa utawala na fedha wa jeshi hilo Mbaraka Semwanza, akizungumza kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa Jeshi la zimamoto na uokoaji Jonhn Masunga wako tayari kushirikiana na chama hicho cha skauti katika masula ya ukozi.

Amesema wamekuwa wakipata ushirikiano mkubwa katika kudhibiti majanga mbalimbali ikiwemo mafuriko licha ya kutokuwa na makubaliano, wanarajia baada ya makubaliano hayo watafanya kazi kwa ushirikiano mkubwa zaidi.

Semwanza ameeleza askari wa Zimamoto wapo wachache hivyo kusaini makubaliano hayo kutawasaidia kuongeza nguvu na tendo muhimu kwa mustakabali wa watanzani.

Amesema wanatarajia baada ya kufikia makubaliano hayo ni kuongeza elewa kwa wananchi kinga katika majanga ya moto lakini pia wamepata mabalozi wa kufanya nao kazi kwa pamoja.

Mapema hivi karibuni katika maeneo mbalimbali nchini kumeripoti matukio ya kuungua kwa mabweni ya shule ambapo kuingiwa kwa mkataba huo utawezesha wanafunzi kupata elimu ya kukabiliana na majanga ya moto.

 

mwisho

Post a Comment

0 Comments