RAIS MAGUFULI AWAPUNGUZIA ADHABU YA KUNYONGA WAFUNGWA 256 .

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli amewapunguzia adhabu wafungwa   256 waliohukumiwa kunyongwa ambapo amesema sasa wapewe kifungo cha maisha.

 Rais Magufuli ametoa msamaha huo leo Disemba 9,2020 wakati akiwaapisha mawaziri na manaibu  mawaziri aliowateuwa hivi karibuni.

 "Kati ya hawa 256 wapo waliohukumiwa kunyongwa kwa sababu ya kuua.  Nimeshindwa kuwaua naomba mnisamehe kwa hilo",amesema Rais Magufuli. 

 "Pia Wafungwa 3316 wa makosa mbalimbali wapunguziwe adhabu na wengine kusamehewa",ameongeza

Post a Comment

0 Comments