RAIS JOHN MAGUFULI AWAAPISHA MAWAZIRI NA NAIBU MAWAZIRI ALIOWATEUWA.

 


📌Na Mwandishi wetu.

 

Novemba 13 aliteua Mawaziri wawili hivyo idadi ya mawaziri walioapishwa kuwa mawaziri kuwa 23 na kusema kuwa kazi ya kuwachagua ilikuwa ngumu kutoka idadi ya zaidi 300.

 "Wote walikuwa wanafaa kupewa uwaziri au unaibu uwaziri. ilikuwa kazi nzito kufanya uamuzi, Kuna vitu vingi ambavyo tumeviangalia katika uteuzi tuliofanya."Alisema Rais Magufuli.

 

Hata hivyo ameongeza kuwa waliochaguliwa sio kwamba ni wazuri sana kuliko wengine, hivyo waende kufanya kazi kwa kuwa watanzania wanataka kuona kazi na wakishindwa yeyote anaweza kuwekwa kwa mbadala.

Ameongeza kuwa "ni nafuu kufanya maamuzi mabaya kuliko kutofanya chochote, fanyeni maaamuzi yatakayo saidia maslahi ya wananchi.

 Suala la ushirikiano ndio jambo la muhimu ili kazi iweze kutekelezeka" na kusisitiza kuwa jambo muhimu ni kusimamia kazi kwa weledi.

 

"Sitaki mitindo ile ya kisasa ya kupiga selfie kwa kila unachofanya, unapaswa kufanya kazi na ajenda nyingine ni za siri .

 

''Teknolojia mpya ni nzuri lakini ni muhimu kwa kuzingatia maadili ya kazi zenu.Ndani ya serikali ni vyema kufanya kazi kwa uadilifu , kuna makundi mengi katika mitandao ya kijamii .

Ndani ya serikali ni vyema kuzingatia siri na maadilli tulio nayo. Idara zote ni muhimu katika taifa letu. Amesema Magufuli

 Katika orodha iliyotangazwa leo baadhi ya mawaziri wamerejea katika nafasi zao, wengine wakipanda kutoka manaibu waziri na kuwa mawaziri kamili,huku kuna sura mpya zilizojitokeza kwenye baraza hilo, halikadhalika baadhi ya mawaziri katika baraza lililopita wakihamishiwa katika wizara nyingine.

 

Mawaziri waliosalia katika nafasi zao ni Profesa Joyce Ndalichako (Elimu), Dotto Biteko (Madini), Jenista Mhagama (Ofisi ya Waziri Mkuu), Selemani Jaffo (Tamisemi) na George Simbachawene (Mambo ya Ndani).

 Wengine waliorejea kwenye nafasi zao ni Mwigulu Nchemba (Sheria), William Lukuvi (Ardhi), George Mkuchika (Utumishi), Medard Kalimani (Nishati).

 

Baadhi ya mawaziri wa awamu iliyopita wamerejea lakini wamehamishwa wizara; nao ni Ummy Mwalimu ambaye sasa ni Waziri wa Muungano na Mazingira kutoka Wizara ya Afya na Innocent Bashungwa ambaye sasa ameteuliwa kuongoza wizara ya Habari na Michezo akitoka Wizara ya Viwanda.

 

Waliokuwa Manaibu Mawaziri na sasa wamepanda na kuwa Mawaziri kamili ni Dkt Damas Ndumbaro (Maliasili na Utalii), Dkt Faustine Ndungulile anayesimamia wizara mpya (Mawasiliano na Teknolojia) , Elias John Kwandikwa ( Ulinzi) Mashimba Ndaki (Mifugo na Uvuvi) na Juma Aweso (Maji).

 Sura mpya zilizopenya ni Prof Kitila Mkumbo (Ofisi ya Rais, Uwekezaji), Prof Adolph Mkenda (Kilimo), Geofrey Mwambe (Viwanda na Biashara)

Sura nyingine mpya ni waliokuwa makatibu wakuu ambao sasa wameteuliwa kuwa mawaziri; nao ni Dkt Leonard Chamuliho (Ujenzi na Uchukuzi) na Doroth Gwajima (Afya).

 Watuele hao wanatarajiwa kuungana na Profesa Palamagamba Kabudi (Mambo ya Nje) na Dkt Philip Mpango (Fedha na mipango) ambao tayari wameshaapishwa.

Wateule hao wanatarajiwa kuapishwa Juma lijalo.

 

Post a Comment

0 Comments