📌FAUSTINE GIMU.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli leo Disemba 24,2020 amemwapisha kamishna wa Maadili Jaji Sivangilwa Mwangesi huku akitoa maagizo kwa watumishi wote kuhakikisha wanakamilisha kujaza fomu za maadili ya utumishi wa umma kabla ya tarehe 30,Disemba ,2020.
Akizungumza mara baada ya uapisho huo
uliofanyika katika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma Rais Dkt. John Pombe
Magufuli amesema kuwa ifikapo Disemba 30,2020 watumishi wote wahakikishe
wanakamilisha kujaza fomu kabla ya Tarehe ,30,2020.
Niwaombe wafanyakazi wenzangu ambao ambao wana wajibu kujaza hizi fomu mhakikishe mnajaza kabla ya Tarehe 30,Disemba,2020 ili zimfikie kamishna mpya kwa sababu sasa hakuna tena sababu ya kisingizio nimejua wengi hatujapeleka fomu hata mimi hapa sijapeleka fomu sasa nitaijaza harakaharaka ili niweze kukufikishi a hizo fomu kwa taratibu za nchiamesema.
Aidha,Rais Dkt.Magufuli ametoa maagizo kwa
tume ya Maadili kuacha kurudisha fomu kwa njia ya mtandao ili kuepuka
wahalifu wa mtandao wanaoweza kughushi na kuleta mtafaruko.
Nilimweleza Marehemu na tulikuwa tumekubaliana kwamba fomu unaweza kuzidownload kwenye mtandao lakini ukishazijaza usirudishe tena kwenye mfumo wa mtandao mtu akishajua ile program anaweza kuedit [kuhariri]na hapa wapo wengi umejaza milioni 10 mtu anakuja kukujazia milioni 100 halafu wewe unakuja kuulizwa ulijaza milioni 100 hapa na originality inapotea msikubali kamwe kurudisha fomu kwa njia ya mtandaoamesema.
Kamishna wa maadili Sivangilwa Mwangesi
ameahidi kutekeleza majukumu yote aliyopewa kwa kufuata miongozo ya nchi.
Akitoa Salam za pongezi,Naibu katibu mkuu Wizara ya katiba ba
Sheria Amon Mpanju ameomba mhimili wa Mahakama kuongezewa nguvu kwa
kuongeza majaji huku Naibu Waziri wa Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora Deogratius Ndejembi amebainisha kuwa mpaka
sasa karibia asilimia 92 ya watumishi wa umma wanajaza fomu za utumishi wa umma
na kutaja mali zao.
Ikumbukwe kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli amemteua Jaji wa Mahakama ya Rufani Sivangilwa Mwangesi kuwa Kamishna wa Maadili kuanzia Tarehe 23 Disemba 2020 ambapo Jaji Mwangesi anachukua nafasi ya Marehemu Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufaa Harold Nsekela aliyefariki Dunia hivi Karibuni.
MWISHO.
0 Comments