POLISI MWANZA YACHUNGUZA MATUKIO MATATU TOFAUTI, LILE LA ASKARI WA JWTZ KUMPIGA MWAMUZI WA SOKA LIMO.


 

Jeshi La Polisi Mkoa Wa Mwanza Linawashikilia Watu Watano Kwa Tuhuma Za Makosa Mbalimbali Yaliyotendeka Kuanzia Tarehe 1 /12/ 2020.


Katika Tukio La Kwanza
Tarehe 01.12,2020 Majira Ya 11:00hrs Katika Mtaa Wa Msumbiji, Kata Ya Kawekamo, Wilaya Ya Ilemela, Vicent Renatus, Miaka 17, Mhaya, Mwanafuzi Wa Kidato Cha Pili, Shule Ya Sekondari Katunguru Na Mkazi Wa Mtaa Wa Msumbiji, Alikutwa Ameuawa Katika Chumba Alichokuwa Akiishi Na Mwili Wake Ukiwa Na Majeraha Shingoni Na Chumbani Kwake Kuporwa Vitu Mbalimbali Vya Nyumbani Ikiwemo Televisioni Na Radio ‘sub Woofer.”

Jeshi La Polisi Mkoa Wa Mwanza Baada Ya Kupata Taarifa Hizo Lilifanya Msako Mkali Ulioongozwa Na Taarifa Za Kiintelijensia  Na Kufanikiwa Kumkamata Mtuhumiwa Aitwaye Hamisi Omary, Nyamwezi, Miaka 19, Mkazi Wa Nyasaka Msumbiji, Ambaye  Baada Ya Kuhojiwa Kwa Kina Alikiri Kuhusika Na Mauaji Ya Mwanafunzi Huyo. Na Aliwaonesha Askari Vitu Vilivyoporwa Kwa Marehemu Na Kwenda Kuviuza Kwa Erasto Jackson, Muha, Miaka 22, Mkazi Wa Kitangiri Ambaye Naye Amekamatwa Na Kuhojiwa Kwa Tuhuma Za Mhalifu Sugu Wa Kupokea Mali Za Wizi. Jeshi La Polisi Mkoa Wa Mwanza Linaendelea Na Uchunguzi Wa Kina Ili Kubaini Wahusika Wengine Wa Tukio Hili.

Hata hivyo katika Tukio La Pili
Tarehe 05.12.2020 Majira Ya 16:50hrs Katika Mechi Ya Mpira Wa Miguu Ligi Daraja La Kwanza Kati Ya Timu Ya Pamba Na Rhino Rangers Ya Tabora, Iliyofanyika Katika Kiwanja Cha Mpira Cha Nyamagana, Kilichopo Wilaya Ya Nyamagana, Jeshi La Polisi Mkoa Wa Mwanza Limemkamata Na Kumuhoji  Askari Wa Jeshi La Wananchi Wa Tanzania Mt.85507 Cpl Silvanus  Silvester @james, Miaka 37, Mhaya, Mkazi Wa Tabora, Kwa Kosa La Kumshambulia Kwa Kumpiga Mateke Na Kichwa Mwamuzi Wa Mpira Wa Miguu Aitwaye  Fadhili Maka, Miaka 33, Mkinga, Mristo, Mkazi Wa Kagera Na  Kuharibu Camera Ya Mwandishi Wa Habari Aina Ya Canon Mali Ya Abdallah Chausiku, Miaka 27, Mkerewe, Mkazi Wa Kiseke. Upelelezi Wa Shauri Hili Unakamilishwa.

 Inaelezwa kuwa katika Tukio La Tatu
Tarehe 05.12.2020 Majira Ya 17:00hrs Maeneo Ya Kamanga, Wilaya Ya Sengerema, Jeshi La Polisi Mkoa Wa Mwanza Limekamata Watu Wawili Waliokuwa Wakijitambulisha Kwa Watu Mbalimbali Kuwa Wao Ni Watumishi Wa Serikali Idara Ya Usalama Wa Taifa Kitengo Cha Afisa Kipenyo, Watuhumiwa Hao  Ni Severine Edward @mayunga,miaka 32, Msukuma, Mkulima, Mkazi Wa Kishiri Ambaye Amekutwa Na Kitambulisho Kilichoandikwa“severine  Edward Mayunga, Jamuhuri Ya Muungano Wa Tanzania Idara Ya Usalama Wa Taifa, Kitengo Cha Kikosi Maalumu Code Mt 82863, Nafasi Under Cover”.na Abel Shiwa@ Mboja, Miaka 46, Msukuma, Mkulima Na Mkazi Wa Kishiri .baadaya Mahojiano Ya Kina Watuhumiwa Wamekiri Kuhusika Na Makosa Ya Kitapeli / Kujipatia Pesa Kwa Njia Ya Udanganyifu . Watafikishwa Mahakamani Haraka Iwezekanavyo.

Kufuatia matukio hayo Jeshi La Polisi Mkoa Wa Mwanza Linaendelea Kutoa Wito Kwa Wananchi Kuendelea Kutoa Taarifa Zinazohusu Wahalifu Na Uhalifu  Ili Zifanyiwe Kazi Kwa Haraka Na Watuhumiwa Waweze Kukamatwa Kabla Hawajatenda Makosa


Post a Comment

0 Comments