📌RAMADHANI HASSAN.
KUTOKANA na mvua zinazoendelea
kunyesha nchini watanzania wameshauriwa kupanda miti ya matunda na vivuli ili
kulinda na kutunza mazingira.
Hayo yameelezwa leo,Desemba
23 Jijini Dodoma na Mtunza fedha wa kikundi cha kutunza na kuhifadhi
mazingira cha ‘Chapakazi’ Darwesh Saidi alipokuwa akizungumza na
Waandishi wa Habari.
Kikundi hicho cha Chapakazi
kinajishughulisha na uuzaji wa miche ya matunda na vivuli ambapo
kinapatikana katika eneo la barabara ya Iringa Mkoani Dodoma.
Darwesh amesema kutokana na
mvua zinazoendelea kunyesha nchini watanzania wanatakiwa kupanda miti ya
matunda na vivuli ili kuweza kutunza mazingira.
“Hapa kwetu kuna miche ya kila aina na tumekuwa tukiwapandia watu garden sasa huu ndio wakati wa kupanda miche ya kila aina ili iweze kuota vizuri lakini pia na kutunza mazingira,”amesema Darwesh.
Amesema katika kikundi
chao,miche ya matunda inayopatikana ni pamoja na Miembe,Michungwa,Miparachichi
na Milimao,
Ameitaja miche mingine
iliyopo ni pamoja na Miche ya kimvuli,ambayo ni
Mitimaji,Miarobaini,Mitingia na Codian,Miche mingine iliyopo ni ya
mbao ambayo ni Greveria,Mitiki,
Kwa upande wa maua amesema
yaliyopo ni Biscas,Exola,Jesus,Lamanda,pamoja na Maua aina ya Parma ambayo
ni Royal Palm,Travell Parm na Golden Parm.
Darwesh pia amesema katika
eneo lao hilo kunapatikana vyungu vya kila aina vikiwemo vinavyotengenezwa kwa
vigae.
“Pia katika eneo hili watu
wanapiga picha kwa ajili ya kumbukumbu pamoja na maharusi lakini tumekuwa
tukitembelewa na wadau mbalimbali,”amesema.
0 Comments