📌NA MWANDISHI WETU;
Aliyekuwa Jaji Mstaafu wa Mahakama ya
Rufani ya Tanzania na Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma
Mhe. Harold Nsekela ameagwa rasmi jijini Dodoma huku Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania akiongoza zoezi hilo.
Mwili wa marehemu Jaji Harold
Nsekela umeagwa katika viwanja vya Chinangali leo huku viongozi wa juu wa
serikali ,wafanyakazi wenzake, wabunge, mawaziri sambamba na mawaziri wateule
wakiudhuria zoezi hilo.
Marehemu Jaji Mhe. Harold Nsekela alifariki
Dunia tarehe 06/12/2020 asubuhi, mjini Dodoma baada ya kuugua kwa muda Mfupi na
mwili wake unatarajia kuwasili mkoani Mbeya katika viwanja vya Songwe majira
saa nane mchana kwa ajili ya mazishi yatakaofanyika siku ya Alhamisi
10/12/2020.
Marehemu Jaji Harold Nsekela
aliteuliwa kuwa Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma mwezi
Desemba, 2016, wadhifa aliokuwa nao mpaka alipofariki.
0 Comments