Mwenyekiti wa mtaa wa
chinyoyo Kata ya kilimani jijini Dodoma Faustina Bendera amewataka wananchi wa
mtaa wa chinyoyo kuelekea sikukuu ya kumaliza mwaka na kuingia mwaka mpya
washerekee kwa amani na wajihadhari katika mkesha wa mwaka mpya kutochoma
matairi na kupiga fataki katika mkesha huo.
alikuwa akizungumza katika mahojiano maalum na mtandao huu mapema leo .
Pia amewakumbusha wananchi wa mtaa huo kuwa baada ya sikukuu hizi mbili watambue kuwa shule zitafunguliwa hivyo kunamaandalizi ya watoto kwenda shule hivyo lazima wawaandae watoto wao mapema kwa maandalizi ya shule
"Na kwa wale
wazazi ambao watawaficha watoto wao kutokwenda shule nitawachukulia hatua kali
za kisheria maana Kuna tabia ya wazazi kuwazuia na kuwaficha watoto wasiende
shule bila sababu wajue tutawashulikia maana serikali ya awamu ya tano imetoa
elimu bila malipo hivyo hakuna Sababu ya kutawapeleka watoto shule"amesema
Faustina
0 Comments