Barua hiyo imesema
kuwa baadhi ya wakimbizi wananyanyaswa na kurejeshwa kwao bila kufuata
utaratibu maalum ndio maana wanaomba taifa lingine liweze kuwapokea.
Lakini mwanzoni mwa
mwezi huu shirika la kutetea haki za binadamu Human Watch, ilitoa ripoti ya
kukemea jambo hilo la kuwa Tanzania inawanyanyasa wakimbizi na kulitaka taifa
hilo liwalinde kwa kufuata sheria za kimataifa.
Wakimbizi hao
wanasema kuwa wameambiwa kuwa wanapaswa kurudi kwao kwa sababu sasa hivi taifa
la Burundi liko salama.
Hata hivyo hapo
nyuma, serikali ya Burundi na Tanzania zilifikia makubaliano ya wakimbizi
kurudi nyumbani kwa kuwa kuna amani kwa sasa ingawa wakimbizi wenyewe wanasema,
si serikali yoyote kati ya hizo mbili ndio wana haki ya kusema usalama upo au
haupo.
Msemaji mkuu wa
serikali ya Tanzania , Dkt Hassan Abas alisema hawajapokea barua yeyote kutoka
kwa wakimbizi, "kama kuna changamoto yeyote kwenye usimamizi wa wakimbizi
Tanzania kuna ofisi za shirika la umoja mataifa linalosimamia haki za
wakimbizi, serikali ipo ,hizo changamoto tungeletewa na kuzitatua".
Aliongeza kusema
"Tunachokisisitiza kuwa Tanzania haiwezi kuwatesa wakimbizi , Tanzania
haiwezi kumdhuru mkimbizi, ambaye sisi wenyewe ndio tulimkubali, tungeweza
kumkataa lakini tumemkubali na akapata kinga ya kimataifa ya kukaa nchini kwetu
mpaka itakaporejea kuwa na amani, sasa tunashiriki vipi kumuhujumu."
0 Comments