📌NA HAMIDA RAMADHANI.
KAMISHNA wa Uhifadhi wa Tanapa Dkt Allan Kijazi amesema kuwa kuna dalili za kuibuka wimbi jipya la ujangili wa tembo ambalo linahamasishwa na watu wachache wenye nia ya kuwahamasisha wananchi na kuwajengea imani kuwa maini na mafuta ya tembo yanasaidia kuponya kansa ya ini,kansa ya kizazi kwa wakinamama na vidonda vya tumbo.
Ameyasema hayo wakati
akifungua mkutano wa Tanapa na Wahariri wa vyombo vya habari na kusema kuwa
kutokana na kuaminishwa huko baadhi ya wananchi wameanza kutumia mbinu za
kuweka sumu kwenye maboga na misumari kwenye maeneo wanayopita ili kuweza
kupata maini na mafuta.
Amesema kuwa
lakini pia pindi wanapowaua tembo hao,wanaofanya kampeni hizo wananunua meno ya
tembo hao nakutoa rai kwa wananchi kuwa hakuna ushahidi wowote wa kitaalam
unaoonyesha kwamba maini na mafuta ya tembo yanatibu magonjwa yaliyotajwa.
Hizo ni mbinu
zinazotumika kuwadanganya wananchi ili wawatumie kufanikisha bioashara ya meno
ya tembo.
Natoa onyo kuwa
hatutasita kumchukulia hatua mwananchi yeyot bila kujali uwezo wake au nafasi
yake katika jamii”amesema.
Amesema kuwa
hifadhi ya serengeti kuchaguliwa kuwa hifadhi bora kuliko zote Afrika na
kupata tuzo ya dhahabu ya ubora wa utoaji huduma kati ya mashirika
51 yaliyochaguliwa kutoka nchi 39 duniani na taasisi inayoitwa European Society
for Quality Research.
Hata hivyo
katika mkutano huo watajadili mikakati ya Tanapa kuhusu utekelezaji wa ilani ya
chama tawala,jinsi walivyojipanga kuboresha utalii has baada ya
janga la homa ya mapafu Covid-19.
Naye Mhariri wa
gazeti la Jamhuri Mkinga Mkinga amesema kuwa ujangili kwa sasa umekuja kwa njia
tofauti hivyo kuna kazi kubwa ya kuhakikisha tunapambana katika kutokomeza
ujangili kwenye hifadhi za taifa.
“Kwa upande wetu
sisi waandishi hatutaishia kuandika tu bali tutahakikisha tunaenda mbele zaidi
iwe kwa kupitia kalamu zetu kuhakikisha tunapiga vita ujangili”amesema.
Mwisho.
0 Comments