📌Na Ramadhan Hassan,Kongwa
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa,DK.Selemani Serera amewaongoza,Wakazi wa Wilaya ya Kongwa kupanda miti zaidi 5000 kandokando ya barabara ya Mbande-Kongwa kwa lengo la kutunza mazingira katika Wilaya hiyo.
Akizungumza leo,Desemba 9 Jijini hapa,wakati wa zoezi hilo,Dk.Serera ambaye alikuwa ameambatana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kongwa,Dk.Omari Nkullo na wafanyakazi wa Halmashauri hiyo amesema miti hiyo iliyopandwa ni lazima itunzwe ili iote na kuifanya Kongwa kuwa ya kijani.
Zoezi hilo pia lilifanywa na wanafunzi wa shule za
msingi na sekondari pamoja na Wananchi wa Kongwa.
"Kupanda miti ni jambo moja na kuitunza ni jambo
lingine nawaomba sana muitunze miti hii,maana hapa tumepanda na mikorosho kwani
katika eneo letu inastawi.Hapa sihitaji kuona mti unekufa nataka istawi na
kuota yote,"amesema.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kongwa,Dk.Nkullo
amesema wanatekeleza kwa vitendo agizo la Makamu wa Rais la kupanda miti
milioni 1.5 kwa mwaka.
Amesema wamepanda miti hiyo kwa km 37 pembezoni mwa barabara ya
Kongwa-Mbande.
0 Comments