Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii Ruth Minja.📌HAMIDA RAMADHANI
MFUMUKO wa Bei kwa
mwaka ulioishia mwezi Novemba,2020 umepungua hadi kufikia 3.0 kutoka asilimia
3.1 kwa mwaka ulioishia mwezi Oktoba ,2020.
Akiongea na waandishi
wa habari leo jijini hapa Kaimu Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii
Ruth Minja amesema hiyo inamaanisha kuwa, kasi ya mabadiliko ya Bei za
bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Novemba,2020 umepungua
ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Oktoba 2020.
Amesema kupungua kwa
mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Novemba 2020 umechangiwa hasa na
kupungua kwa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula kwa kipindi Kilichoishia
mwezi Novemba,2020 zikilinganishwa na bei za mwezi Novemba,2019.
"Baadhi ya bidhaa
za vyakula zilizopungua bei kwa mwezi Novemba,2020 zikilinganishwa na bei za
mwezi Novemba,2019 nipa moja na Mchele asilimia 4.5, Mahindi asilimia 14.3,Unga
wa Mahindi asilimia 5.7,Unga wa Mtama asilimia 4.4,Viazi vitamiu asilimia 2.6,
vyakula vya Watoto( Lishe) asilimia1.8 na Ndizi za kupika
asilimia 4.9. Ruth Minja.
Ameongeza kuwa mfumoko
wa bei wa bidhaa za vyakula na vinjwaji baridi kwa mwezi Novemba,2020 umepungua
hadi asilimia 2.8 kutoka asilimia 3.4 kwa mwaka ulioishia mwezi Oktoba
2020",amesema.
HALI YA MFUMOKO WA BEI
NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI.
Amesema Nchini Kenya
mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Novemba,2020 umeongezeka hadi kufikia
asilimia 5.46 kutoka asilimia 4.84 kea mwaka ulioishia mwezi Oktoba 2020.
Kwa Upande wa nchi ya
Uganda, Mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Novemba,2020 umepungua
hadi kufikia asilimia 3.7 kutoka asilimia 4.5 kwa mwaka ulioishia mwezi
Oktoba,2020.
0 Comments