📌NAZA KIRIMBO.
MBUNGE wa jimbo la Dodoma Mjini Anthony
Mavunde ametoa wito kwa mafundi ujenzi kuwa na umoja ili kutambulika kwa lengo
la kunufaika na fursa za ujenzi zilizopo jijini hapa.
Mavunde aliyasema hayo
jijini hapa katika halfa iliyoandaliwa Kampuni uzaji wa vifaa vya ujenzi ya
Najel Builders na kuwakutanisha mafundi ujenzi zaidi ya 50.
Alisema kupitia umoja
huo itasaidia kundi hilo kuunganishwa na fursa za ujenzi zinazopatikana jijini
hapa ili kunufaika na uwepo wa Makao Makuu ya nchi, Dodoma.
Mathalan,alisema baada
ya kujiunga au kuunda umoja huo, utawanufaisha, kwanza kwa kuwa na anwani
lakini pia kupata fursa mbalimbali za kutoa huduma ya ujenzi.
“Mkiwa na umoja wenu,
zinapotokea kazi inakuwa rahisi kuwaunganisha, unawaambia tu kuwa nenda sehemu
mflani utapata mafundi wazuri, waaminifu ambao watafanyaka kazi nzuri. Hii
itasaidia hata mmoja wenu akifanya jambo la tofauti awe anapoteza sifa ili
asiwachafue wengine,” alisema Mavunde.
Mavunde alisema pamoja
na kuwa na mafundi wengi jijini hapa,kikubwa ni uaminifu ambayo ni silaha ya
mafanikio.
Alisema wapo watu
hawana mtaji wa fedha lakini wana mtaji wa uaminifu hivyo kupitia uaminifu huo
wamekuwa wakipata kazi nyingi.
Hata hivyo alisema
kupitia umoja huo atawasaidia mafundi hao kupata bima ya afya ili kuwa na
uhakikia wa matibabu.
“Kwa kazi ambazo
mnazifanya ni lazima muwe na bima ya afya, ni lazima tuilinde nguvu kazi yetu.
Na katika hili siku yeyote mkiwa tayari niambieni nitawatafutia mtaalam aje
awaelimishe kuhusu masuala ya bima ya afya sanjari na umuhimu wake,” alisema.
Katika hatua nyingine,
Mkurugenzi mtendaji ya Kampuni ya Najel Builders Neema Nzwalile alisema
kutokana na changamoto ya wajenzi wengi Dodoma kukosa mafundi na ushauri wa
kitaalamu kampuni hiyo iliamua kutafuta suluhisho la tatizo hilo.
Nzwalile alisema
waliamua kumrahisishia mjenzi kupata vifaa na mafundi pamoja na ushauri wa
kitaalamu kuhusu masuala ya ujenzi.
Alisema Dodoma inakua
kwa kasi na katika ukua huo inahitaji mafundi ambao wanafanya kazi vizuri
ambapo ili kufikia lengo hilo wameamua kuwakutanisha mafundi kwa lengo la
kuunda umoja wao.
Alisema lengo ni
kuwaunganisha mafundi wote ili wanufaike na fursa zilizopo jijini hapa.
Naye mwenyekiti wa
mafundi hao Wille Sakalani alitoa shukrani kwa ahadi zilizotolewa na mbunge
huku akisema malengo yao ni kufikia hatua ya kusajili kikundi ili
waweze kunufaika na fursa mbalimbali ikiwamo mikopo.
Mwisho.
|
|
0 Comments