📌Na DEVOTHA SONGORWA.
SERIKALI imeyataka
Mashirika na Taasisi mbalimbali zinazoratibu miradi ya wakulima kusimamia
miradi yao katika mfumo unaotambulika na serikali ili kusimamia na
kulinda haki za wakulima kukomesha ubabaishaji katika sekta ya kilimo.
Hayo yamesemwa na
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Mazao,Wizara ya Kilimo, Nyasebwa Chimagu wakati wa
ufunguzi wa mkutano wa siku mbili wa mbegu za asili na vyakula vya asili
uliokutanisha wakulima,wadau wa kilimo kutoka mikoa mbalimbali ikiwemo
Shinyanga,Iringa Mwanza,Mbeya na Dodoma ukilenga kuwajengea uwezo wakulima
namna ya kutunza na kuendeleza uzalishaji wa mbegu bora za asili.
Amesema kama Wizara
inao mfumo rasmi wa mbegu unaosimamiwa kwa mujibu wa sheria ya mbegu
kuhakikisha usalama wa mkulima tangu kupanda hadi kuvuna kuondokana na madhara
yanayoweza kujitokeza.
“Ni lazima miradi hii
iratibiwe kwa mfumo wa wazi na kwa utaratibu ijulikane kama ni mbegu
inapatikana wapi tusifanye kama maonesho mbegu iko wapi,imeisha tunakuwa
tunafanya siasa tunataka tujue maeneo gani mbegu zinapatikana tunataka tuongeze
tija katika kilimo”,alisema Mkurugenzi huyo.
Pia Chimagu amewataka
wadau kuwapa elimu wakulima ya namna ya kuongeza thamani ya malighafi
zinazopatikana katika maeneo yao kutengeneza mbolea za asili,kuzalisha pembejeo
zinazotakiwa na mbegu bora kwa kilimo.
“Tuepuke siasa katika
kilimo kuwe na mashamba darasa wafundishwe kilimo biashara na katika kilimo hai
lazima tuhakikishe tunatunza mazingaira na naoimba tushieikiane kwa pamoja
kuunda miongozo nimeona meza zenu kuna soya, mahindi, maharage, karanga
tudumishe vyakula vyetu vya asili vinatusaidia kuepuka magonjwa”,alieleza
Chimagu.
Kwa upande wake
Mhadhiri wa Chuo kikuu cha Dar es salaam (UDSM) ambaye pia ni mtaalamu wa
kilimo na mazingira,Prof Agness Nyomora amesisitiza jamii kutumia vyakula vya
asili kujenga afya zao na kuepuka magonjwa huku akiwataka wakulima kuzingatia
maelekezo ya wataalamu wa kilimo.
“Kumeibuka maradhi
lukuki ambayo hata hatuelewi yanatoka wapi lakini mengine tunasababisha sisi
tumeacha vyakula vya asili tunapenda vya kusindikwa turudi edeni na wakulima
nao wafuate ushauri wanaopewa wa dawa sahihi ,mbegu bora, mbolea za asili wengi
wanajali pesa hawangalii mlaji ataathirika vipi”alihimiza Prof.Nyomora.
Naye Mjumbe wa bodi ya
Shirika lisilo la kiserikali la Tanzania Organic Agriculture Movement (TOAM)
Henry Mgingi ameeleza kwamba lengo la mkutano huo ni kuwajengea uwezo
wakulima na wadau namna ya kutambua mbegu bora za asili kuepuka kuuziwa mbegu
zisizofaa kutoka nje ya nchi au ndani ya nchi huku akiiomba serikali kusimamia
sera za mbegu.
“Dira ya Taifa ya
maendeleo ya mwaka 2020-2025 tunaamaini kila mtu atakuwa katika hali nzuri ya
maisha na yote haya yanaanzia kwenye mbegu tunataka kuimarisha uhuru wetu kama
waafrika na watanzania tunapiga vita mbegu hatari tunazoletewa wakati sisi
wenyewe tuna uwezo wa kuzalisha na kuziendeleza tuchukue kama mhimili wa maisha
yetu ya kila siku,”alisema Mgingi.
Aidha Esther Ihano ambaye
ni mkulima kutoka Mwanza ameishukuru Serikali kwa kuendelea kuweka sera zinazolinda
maslahi ya wakulima na kufanya sekta hiyo kuheshimika katika jamnii akiwataka
watanzania kubadili mtindo wa maisha na kutumia vyakula vya asili.
"Mimi Ni mkulima wa
mahindi,maharage,karanga najivunia kutumia mbegu za asili maana zinastahimili mazingira
na hali ya hewa ya kwetu Tanzania na Serikali imekuwa mstari wa mbele
kututetea",alisema Esther.
0 Comments