KUNA MAZINGIRA RAFIKI YA UWEKEZAJI DODOMA;

📌Na JASMINE SHAMWEPU.

MKUU wa Wilaya ya Dodoma Josephat Maganga, amesema kuwa mkoa wa Dodoma unaendelea kuweka mazingira rafiki na wezeshi kwa wawekezaji kuwekeza katika maeneo mbalimbali ikiwa ni sehemu ya kutekeleza agizo la Rais John Magufuli.

Mkuu huyo wa Wilaya, ameyasema hayo jijini Dodoma, wakati alipokuwa akizindua maduka ya GSM ya nguo na samani za maofisi na majumbani.

Maganga, amesema kuwa serikali hivi sasa imeondoa urasimu pamoja na milolongo mirefu kwa wawekezaji ili kuwezesha upatikanaji wa vibali kuchukua muda mfupi kama ambavyo Rais aliagiza wakati akizindua Bunge la 12.

 Pia, amesema GSM, wamefanya uwekezaji huo katika kipindi mwafaka kwani jiji la Dodoma lilikuwa linahitaji huduma hizo kwa muda mrefu.

 Aidha, ameitoa wito kwa wawekezaji mbalimbali kujitokeza kuja kuweza jijini Dodoma kwani bado yapo mahitaji mengi.

Amesema, jiji la Dodoma bado linayo ardhi ya kutosha kwa ajili ya kuwekeza huduma mbalimbali kama vile sekta ya afya, elimu, miundombinu pamoja na viwanda.

 Kwa upande wake mtendaji mkuu wa GSM, Fatuma Abdallah, amempongeza Rais Magufuli kwa kuweka mazingira rafiki kwa wawekezaji.

Amesema Hali hiyo itasaidia kuongeza wawekezaji wengi kutokana na mazingira rafiki yaliyopo ikiwemo agiza la Rais kutaka vibali vya wawekezaji kutolewa ndani ya siku 14.

 


Post a Comment

0 Comments