KILIMO CHA KISASA KUONGEZA UZALISHAJI WA ZABIBU HADI 50%.



📌Na Saleh Ramadhani.

 IMEELEZWA kuwa mbinu bora za uzalishaji wa zao la zabibu  una uwezo wa kumuongezea mkulima ongezeko la faida hadi kufikia asilimia 50% katika kipindi cha msimu wa mavuno.

 Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Kituo cha utafiti  wa zao la Zabibu (TARI) - Makutupola  Dkt. Cornel Massawe mara baada ya waandishi wa habari za kisayansi na Watafiti kutoka  Mikoa ya Dodoma na Singida walipotembelea kituo hicho kilichopo Makutupora Mkoani Dodoma.

 Dk Masawe amesema  shilingi  millioni 297 za kitanzania zimetengwa kwa ajili ya kuboresha Kilimo cha zabibu katika Taasisi hiyo ya utafiti,fedha ambazo zimetolewa na Serikali kupitia  TUME ya Taifa ya Sayansi na teknolojia Nchini (COSTECH).

 Fedha hizo zimelenga kuongeza tija Katika zao la zabibu nchini ikiwa ni Pamoja na kuendesha ujenzi wa kiwanda kidogo cha kuchakata zao hilo.

 "fedha hizi tumekuwa tukitoa mafunzo ya Kilimo cha zabibu kwa wakulima wadogo wadogo wa zao la zabibu jijini hapa ili kukuza Kilimo  na kukiongezea thamani ,"

Amesema Dkt.Massawe.

 Hata hivyo,amefafanua kuwa kiwanda hicho kinatumika kuchakata Zabibu kwa ajili ya kutengeneza Juice na Mvinyo,sanjari na kutoa mafunzo kwa wakulima na wafanyabiashara wa bidhaa hizo ambao wamekuwa wakitembelea kituoni hapo kama shamba darasa.

 Kwa upande wake mtafiti wa Idara ya Udongo kituoni hapo Ashura Ally amesema kuwa wamekuwa wakitoa mafunzo kwa Wakulima hao kuanzia uandaaji wa mashamba hadi kufikia uvunaji wa zao hilo.

 Amefafanua kuwa wakati wa kuandaa Shamba la Zabibu lazima uangalie Udongo,Shamba liwe Safi,kupanda miche kwa mpangilio pamoja na kuzingatia vipimo vya mbolea na Udongo.

 "TARI tuko hapa  kwaajili ya kuwasaidia wakulima hivyo tunapenda kuwakaribisha wakulima wote wanaohitaji kujifunza kwa makundi na mtu  mmoja anakaribishwa" 

 Ashura Ally.

Kwa Mujibu wa Mtafiti Idara ya  uhailishaji na usambazaji wa Teknolojia TARI Makutupola  Stella Hambangabe mkoa wa Dodoma ni sehemu pekee katika Kilimo hicho.

 " Zao la Zabibu ni fahari ya Dodoma kwani hali ya hewa ya hapa inakuza Kilimo cha  Zabibu hivyo ni vema kila mmoja ajikite kuendesha kilimo hicho,"' amesema.

 Mbali na faida lukuki na kutumika kama zao kuu la biashara, zabibu huondoa tatizo la kukosa choo,mmeng'enyo wa chakula kwenda vizuri na kupunguza uchovu mwilini.

 Mwisho.

 


Post a Comment

0 Comments