Kikundi
cha kutunza na kuhifadhi Mazingira cha
(Chapakazi) cha Jijini hapa kimetoa zawadi ya mwaka mpya kwa wateja wake ambayo
ni punguzo la bei ya Miche ya matunda na
vivuli lengo likiwa ni kuendelea kulifanya Jiji la Dodoma kuwa la kijani.
Hayo
yameelezwa leo Jijini hapa na Mtunza Fedha
wa Kikundi hicho,Darwesh Said alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari.
Darwesh amesema kutokana na dhamira ya Kikundi hicho kuwa ni kuhakikisha Dodoma inakuwa ya kijani imetoa punguzo la asimia 20 ya miche yote inayouzwa katika eneo lao lilopo barabara ya Iringa.
Amesema
Miche ya Miembe ambayo awali ilikuwa ikiuzwa kwa shilingi 5000 sasa itauzwa kwa
shilingi 4000.
Darwesh
amesema Miche ya Miparachichi,Michungwa,Mindimu na Milimao iliyokuww
ikiuzwa kwa shilingi 5000 sasa itauzwa kwa shilingi 3000
Kwenye
miche ya vimvuli amesema itauzwa kwa shilingi 2000 ambapo awali ilikuwa ikiuzwa
kwa shilingi 3000.
Hata
hivyo,Darwesh amewaahidi wakazi wa Dodoma wataendelea kupata miche bora kutoka katika Kikundi hicho
kwa mwaka ujao wa 2021.
"Kwanza
tunawatakia Sikukuu njema,kikubwa tunawahamasisha kuendelea kupanda miti ili
kutunza mazingira,ahadi yetu kwa wateja wetu ni tutaendelea kuhamasisha
upandaji wa miti,na sisi tunawaomba Watanzania wapande miti,"amesema.
Mwisho
0 Comments