KATIBU MKUU WA CCM DKT. BASHIRU AKUTANA NA BALOZI WA CHINA WANG KE .



📌NA HAMIDA RAMADHANI 

KATIBU Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt Bashiru Ally amekutana na Balozi wa China nchini Tanzania  Wang Ke na kujadili Maendeleo na mashirikiano baina ya nchi ya Tanzania na China.

 Akiongea na waandishi wa habari katika viwanja vya makao makuu ya CCM Jijini Dodoma  maarufu (white house) Katibu Mkuu Dkt Bashiru Ally amesema agenda kuu  katika kikao hicho cha muda mfupi  nikuona namna ya kuendeleza ushirikiano Kati ya chama cha China na chama cha CCM.

Amesema katika kikao hicho na balozi Wang Ke alimkabidhi Ilani ya chama cha Mapinduzi (CCM) pamoja na hotuba mbili ambayo ya kwanza ni utendaji kazi ya serikali ya awamu ya Tano,huku hotuba nyingine ikiwa ni ile ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli kulifunga bunge.

“Tunaimani kuwa ushirikiano uliopo kati ya nchi ya China na Tanzania ni mzuri na urafiki huu utadumu” amesema Dkt Bashiru.

Kwa Upande wake Balozi wa China nchini Tanzania Wang Ke  ameipongeza serikali ya Tanzania kwa kufanya uchaguzi Mkuu wa uliomalizika October 28/2020 kwa kutumia fedha za ndani.

"Kwa mara ya kwanza Tanzania imeweza kuendesha na kufanya uchaguzi Mkuu kwa kutumia fedha za ndani bila kutegemea fedha za wahisani kwa jambo hilo hongereni Sana," amesema Balozi Wang Ke.

Hata hivyo ameipongeza serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya Rais wake Dkt Hussein Mwinyi kwa kuwa  na mashirikiano mazuri na chama cha ACT Wazalendo.

 

 

 

 

Post a Comment

0 Comments