JESHI la Polisi Mkoani Dodoma
linawashikilia watu wanne kwa tuhuma za unyang’anyi wa kutumia silaha
baada ya kupatikana wakiwa na Bunduki mbili aina ya Shotgun
zilizotengenezwa kienyeji mfano wa pisto pamoja na risasi tano za bunduki aina
hiyo.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo Jijini Dodoma Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma
Gilles Muroto amesema kuwa Jeshi hilo limefanikiwa kukamata watuhumiwa hao
baada ya kufanya oparasheni mbalimbali kwakushirikiana na Jeshila Polisi Mkoa
wa Morogoro ambapo mnamo Desemba 23 Mwaka huu maeneo ya Chalinze nyama Wilayani
Chamwino Michael John alikutwa na risasi tano za shotgun wakijiandaa kufanya
unyang”anyi baada ya kuhojiwa alikiri na kuwataja wenzake.
Aidha,Kamanda
Muroto amesema kuwa watuhumiwa hao wamekuwa wakifanya uhalifu katika maeneo
mbalimbali ya Mkoa wa Dodoma na Morogoro ambapo Disemba 19 mwaka huu walifanya
uhalifu Kijii cha Izava baada ya kuvamia Duka na kumjeruhi mwenye
duka kwa risasi na kupora fedha kiasi cha Sh milioni30 na simu 40.
Kamanda
Muroto amesema kuwa wamewakamata watuhumiwa saba ambao ni wakazi wa Dodoma
baada ya kukutwa na vifaa mbalimbali ambavyo vizaniwazo kuwa ni za
wizi zikiwemo kompyuta,televisheni printer na muziki sistimu.
Katika hayua nyingine kuelekea
Sikukuu ya Krismas Kamanda Muroto amesema Jeshi limejipanga kuimarisha ulinzi
na usalama wa raia na mali zao ikiwa ni pamoja na kutoa elimu katika nyumba za
ibada ili watu washerehekee kwa amani ambapo linashirikiana na jumla ya
vijana300 kama ulinzi shirikishi amesema madereva wanaobunja sherrtia za
usalama baearabarani watawachukulia hatua za Kisheria.
0 Comments