📌NA SALEH RAMADHANI.
TUME ya haki za
binadamu na utawala bora Nchini(THBUB) imesema imekuwa ikiunda vilabu kwa jamii
kuanzia shule za msingi hadi vyuoni kwa lengo la kutoa elimu ya haki za binadamu
ili Jamii iweze kuachana na mila potofu.
Mila hizo ni zile ambazo
zimeonekana ni chachu ya kukithiri kwa matukio ya unyanyasaji na ukatili wa
kijinsia.
Hayo yamebainisha leo
Jijini Dodoma na Makamu Mwenyekiti wa Tume hiyo, Mohamed Hamad kwenye kongamano
la siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsialililofanyika katika chuo Kikuu cha
Dodoma(UDOM).
Amesema kuwa lengo lao
ni kuwaelimisha,kutambua misingi ya haki za binadamu na utawala Bora ikiwa ni
pamoja na kufanya tafiti ili kuhakikisha jamii inanufaika na haki hizo.
‘’Sisi tume tunaona
kuna mabadiliko makubwa sana katika hali ya haki za binadamu nchini,pia
tunashuhudia uelewa wa watu katika kutambua umuhimu wa haki za binadamu na
kuendeleza misingi yake”amesema.
Amesema bado zipo
changamoto mbalimbali katika jamii hususani ukeketaji,uzalilishaji watoto na
kuzalilishwa kwa wanawake ambapo amsema kuwa wakiwajengea uwezo wanafunzi itakuwa
ni chachu ya mabadiliko na mchango mkubwa katika kupunguza au kuondoa ukatili
wa kijinsia nchini.
‘’tunaamini kwamba
wanafunzi tukiwajengea uwezo mzuri itakuwa ni msingi mzuri katika kutoa mchango
na kuleta mabadiliko katika kupunguza au kuondosha ukatili wa kijinsia kwa
Nyanja tofauti tofauti’’ amesema.
Naye kamishna wa Tume
ya haki za binadamu na utawala bora Dr Fatma rashid halfan amesema kuwa lengo
la kuanda kongamano kwa wanafunzi ni kufanya uchunguzi,kuelimisha jamii na
kufanya utafiti kwa kushirikiana na wanafunzi ili kupata data nyingi za ukatili
wa kijinsia katika jamii.
DK. FATMA ameongeza
kuwa kila mtu anatakiwa kujua haki zake na kutambua kuwa mila na desturi
zinachangia sana kurudisha maendeleo yanchi na jamii itambue kuwa ikizingatia
misingi ya haki na utawala bora masuala ya ukatili wa kijinsia utatokmea kwa
kiasi kikubwa.
Kwa upande wao wanafunzi
wa Chuo Kikuu cha Dodoma akiwemo Rais wa Jumuiya ya wanafunzi wa Haki za
Binadamu Chuo kikuu cha Dodoma(UDOM) Geneus Kato wamekiri kuwepo kwa
vitendo vya ukatili wa kijinsia katika vyuo ambapo amsema kuwa wanafunzi wa
vyuo wanakumbwa sana na ukatili wa kingono huku akisema hawapo tayari kuvumilia
vitendo hivyo kuviacha vikiendelea vyuoni.
‘’matukio ya ukatili
wa kijinsia yanatokea sana vyuoni hususani matukio ya Ngono vyuo nayo ni
matukia yanayotokea sana mara mara,sisi kama jumuiya ya wanafunzi
tunakemea sana matukio yanayotokea vyuoni hususani rushwa ya ngono’’.amesema.
Tume
ya Haki za Binadamu na Utawala Bora ni idara huru ya serikali, iliyoundwa
kama Taasisi ya kitaifa ya kukuza na kulinda haki za binadamu.
MWISHO.
0 Comments