📌 BONIPACE RICHARD.
SUALA la kunawa mikono limekuepo tangu enzi, Nakumbuka
ingali wadogo tulikuwa tukihimizwa kunawa mikono kwa maji safi na salama kwa
kutumia sabuni ili kujikinga na magonjwa ya milipuko yanayo sababishwa na
uchafu hasa unapotoka chooni na pale unapomaliza kula.
Historia hiyo inasadifu kuwa suala la usafi ni sehemu
yetu ya maisha kwani tumekuwa tukifundishwa shuleni utaratibu wa kunawa mikono
kwa maji safi na tiririka ili kujikinga na magonjwa ya mlipuko.
Mtiririko huo unaosadifu kuwa kampeni ya kunawa
mikono kwa maji safi tiririka na sabuni iloianza tangu jadi na kabla ya janga
la ugonjwa unaosababishwa na virusi vya CORONA (Covid 19)
Hata hivyo,utamaduni wa kunawa mikono mara kwa mara
ni muhimu katika Maisha ya kila siku ya mwanadamu, kwani ni njia sahihi ya
kujikinga na magonjwa ya mlipuko yanayo sababishwa na uchafu ikiwemo kuhara,
kichocho kipindupindu nakadhalika.
Magonjwa kama ya kuhara, kipindupindu, kichocho, na
mafua yanayosababishwa na virusi vya Corona ugonjwa wa zika na magonjwa mengine
ya mlipuko yanasababiswa na uchafu huku njia inayoeneza maambukizi hayo ikitajwa
kuwa ni kupitia njia ya hewa pamoja na kugusana.
Aidha,hutegemea hulka ya mtu na mtu katika
kuzingatia usafi wake mwenyewe.
Hata hivyo Kuna baadhi ya watu huzembea kwa makusudi
kutokunawa Kunawa mikono kwa maji safi tiririka na sabuni licha ya kuwepo kwa
elimu dhidi ya kujikinga na magonjwa ya mlipuko yanayosababishwa na uchafu.
JAMII
Kwa Upande wa Jamii hasa wakazi wa mkoa wa Dodoma,kuhusiana
na hali ya unawaji mikono katika kuhakikisha wanajikinga na magonjwa yanayosababishwa
na uchafu wamesema kwasasa hawana hamasa kama kipindi cha mlipuko wa mafua
yanayosababishwa na virusi vya Corona.
“hamasa ya unawaji wa mikono huanzia kwenye
familia, shuleni, ofisini na sehemu zote zenye mikusanyiko umepungua”
Akiongea kwaniaba ya wakazi wenzake, Happines
Gwimile Mkazi wa Ipagala jijini Dodoma Amesema hamasa ya unawaji wa mikono kwa
maji safi na tiririka umepungua kwasababu watanzania wameshaondokana na
hofu ya uwepo wa mafua yanayosababishwa na virusi vya Corona.
"Unajua Sisi watanzania tuko hivi
mtanzania akijengewa hofu ni kweli anaingiwa na hofu kwelikweli lakini
mtanzania huyo huyo ukimpa matumaini ya kitu chema na moyo wake unakuwa safi na
haru" alisema Happines
Aidha kutokana na msimamo wa Tanzania kuwa Tanzania haina ungonjwa wa Corona (Covid-19) ndio maana
unawaji wa mikono na uvaaji wa barakoa umepungua kutokana na kujengewa dhana ya
kutokuwepo kwa ugonjwa huo hapa nchini hali inayopelekea Watu kuacha
Kunawa mikono na kuvaa Barakoa.
Ameongeza hii ni changamoto kwetu na hasa Sisi wazazi na wale utakuta mzazi anaelimu ya kutosha juu ya kujikinga na magonjwa ya mlipuko yanayo sababishwa na uchafu na ikiwemo kutonawa mikono kwa maji safi na sabuni lakini tumekuwa wazito kuwafundisha watoto wetu umuhimu wa Kunawa mikono mara kwa mara hata baada ya kutoka chooni, amesema Happines
Amesema licha kuwahimiza watoto kuzingatia usafi ikiwemo unawaji wa mikono lakini pia hata shuleni hakuna miundombini ya
kuwafanya watoto wawe na utaratibu wa Kunawa mikono Kila na baada ya kutoka
kujisaidia.
Anaongeza kuwa, kabla ya mlipuko wa ugonjwa wa
Corona hapa Nchini, utaratibu wa kunawa mikono haukuwepo sehemu katika sehemu
mbalimbali ikiwemo kwenye taasisi zote za serikali maeneo yenye mkusanyiko na
kadhalika.
"Sasa hivi Hali imebadilika hamasa ya kunawa mikono imepungua tofauti na awali na hata ukijaribu kutembea katika
Ofisi za umma na Binafsi, vyuo vya elimu ya juu na shule zote za Msingi na
sekondari miundombinu ya Kunawa mikono hakuna,"
Kwa kuongezea tu, Sehemu nyingine Utakuta
miundombinu ya Kunawa mikono au madumu ya maji yamefunikwa na hakuna maji
wala sabuni" aliongezaHappines
NINI KIFANYIKE
Jambo kubwa la kuzingatia ni elimu ya usafi kutolewa
na miundombinu ifanyiwe kazi pamoja na kuboreshwa kwa kutengenezwa upya kwani
imebainika hivi karibuni kuwa kila sehemu miundombinu ya maji imeharibika hivyo
inatakiwa kutengenezwa upya na kuweka maji ya kutosha ili Watu waendelee na
utaratibu wa Kunawa mikono ili kujikinga na maradhi yatokanayo na uchafu.
"Kuna baadhi ya maeneo wananchi wanachangamoto
ya maji utakuta sehemu ya upatikanaji wa maji ni shida hivyo katika maeneo hayo
serikali na Taasisi ambazo zinahusika na uvunaji wa maji ya mvua wahusishwe
katika kuhakikisha wanawatatulia changamoto hiyo ili wakabiliane na
magonjwa ya mlipuko.
"Hamasa ya unawaji umepungua leo hii ukiamua
kwenda katika Ofisi za Serikali na binafsi nyingi Utakuta madumu ya maji meupe
hakuna maji wala sabuni inatakiwa tuendeleze utamaduni wa unawaji wa mikono
kujikinga na magonjwa mengine yanayotokana na uchafu"
KWA UPANDE WA WANAFUNZI SHULENI
Hapa tunakutana na Ally Shomari Ni mwanafunzi wa
shule ya sekondari ya Mlimwa iliyopo kata ya Miuji jijini hapa anasema suala la
unawaji wa mikono katika shule yao halitiliwi mkazo tofauti na hapo wali.
Anasema kipindi cha Corona, katika shule yao
kulikuwepo na miundombinu ya maji pamoja na madumu ya maji ya kutosha katika
kila darasa ambapo wanafunzi ilikuwa ni lazima Kunawa kabla na baada ya kuingia
darasani.
Aidha tangu tangazo la kwamba Tanzania
hakuna corona madumu ya maji shuleni yalidumu kwa muda wa wiki mbili tu baada
ya hapo madumu ya maji tulipokuwa tukinawia mikono Kwaajili ya kujikinga na
corona yalitolewa.
Mwandishi wa makala hii hakuishia hapo ambapo
amejaribu kupitia katika maeneo tofauti tofauti na hapa tunakutana na Mwalimu
wa shule ya sekondari ya Mtumba Moreen Shitindi anasema katika Mazingira ya
shule yao suala la unawaji wa mikono limepungua tofauti na hapo awali kipindi
cha corona.
Anasema ile Hali ya wanafunzi kuvaa barako,
Kunawa mikono hamasa imepungua tofauti na kipindi cha mlipuko kwani hata watoto
ukiwaelimisha imekuwa vigumu.
"Sisi kama walimu wa Mtumba tunajitahi
kuwasihi wanafunzi Kunawa mikono kuendelea Kunawa mikono lakini muitikio wa
wanafunzi kutekeleza jambo hilo umekuwa ni mgumu kutekeleza," alisema
Mwalimu
Aliongeza kuwa katika Nchi yetu mungu ametupendelea
kwani maombi tuliyoyafanya yametukomboa na janga hili ambapo kwasasa tupo huru
na salama na hili janga limepotelea mbali.
Kwa upande wake mwananchi kutoka Wilaya ya Chamwino
Ikulu Ismail Mbiga amesema ni sawa tu kutokuwepo kwa miundombinu ya maji katika
sehemu zote za mikusanyiko ikiwemo shuleni, ofisini na hata masokonio.
Amesema Mungu amesikia maombi yetu watanzania wote
baada ya kufunga na kuomba kwa muda wa siku Tatu maombi yetu yamefika na
yamekubalika na ndio maana hadi leo hii tuko Salama.
Sanjari na hayo, ameongeza kuwa Nchi ya Tanzania
bado ni Nchi masikini na endapo ingetokea ugonjwa wa Corona ungeendelea hakika
tusingeweza kukabiliana nao kwani hata Nchi kubwa za ulaya zimeshindwa kuzuia
janga hilo ambalo ni tishio kwasasa duniani kote.
Anasema janga hilo ni janga kubwa ambapo nchi zenye
fedha na ambazo zinajiweza kiuchumi zimeshindwa kukabiliana na ugonjwa huu
lakini Tanzania tumefanikiwa na yote ni kutokana na maombiambayo mwenye mungu
aliyapokea na kutunusuru na janga hilo hatari.
"Hivi ndugu mwandishi wa habari unadhani
kama kungekuwa na huu ugonjwa wa Corona Covid-19 Sisi Tanzania tungebakia
mpaka muda huu kweli hakika nakuapia tungeteketea wote kama Kuku,"
amesema Mbiga
MWISHO
0 Comments