HEKARI 350 ZATENGWA KUJENGA CHUO KIKUU DODOMA.

📌DEVOTHA SONGORWA.

KANISA la Waadventista Wasabato nchini linatarajia kujenga Chuo kikuu  ambapo Jumla ya hekari 350 zimepatikana kwa ajili ya ujenzi  utakaoanza mwaka 2021 kama sehemu ya kuunga mkono Serikali katika kuboresha sekta ya elimu.

 Akizungumza na mtandao huu Mkurugenzi Idara ya Elimu Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo Kuu la Kusini mwa Tanzania,Devotha Shimbe amesema Serikali imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha wanafunzi wanasoma katika mazingira rafiki kwa kutatua changamoto zinazojitokeza katika maeneo mbalimbali.

Ameongeza kwamba baadhi ya maeneo wanafunzi wamekuwa wakitembea umbali mrefu kufika shuleni hali inayosababisha   kukosa masomo na hata kujikuta wakiingia katika vishawishi hatimaye hukatisha masomo yao kwa kupata mimba na wengine wakijiunga katika makundi ya uhalifu.

“Kama Union ina mpango wa kujenga Chuo Kikuu katika eneo la Chididimo hapa Dodoma lakini tutaanza na Chuo cha Ufundi ambacho kitakuwa chini ya Veta nia ni kuwezesha vijana kujiajiri kwani watakuwa na ujuzi wao hivyo tutakavyokuja kwenu kufanya changizo maalumu tunaomba mtupe ushirikiano”,alisema Devotha.

Amefafanua kuwa hivi sasa jamii inalalamikia uvunjifu wa maadili hii ikiwa ni kutokana na sababu mbalimbali kama vile ukuaji wa teknolojia lakini bado ipo haja ya kusimamia utamaduni unaojenga akisisitiza wazazi na walezi kutofumbia macho vitendo viovu vinavyofanywa na watoto wao.

“Hakuna sekta muhimu kwa mwanadamu ka elimu na tunaona serikali imefanikisha nyanja ya elimu bure imeongeza mwamko wa wazazi kupeleka watoto shule na wakati tunafanya hivyo tusiache kufundisha watoto wetu kumjua Mungu tukiwandaa kuwa watumishi wema katika maisha yao”,alifafanua Devotha.

Aidha aliwashauri waumini wa   kanisa hilo kuchangamkia fursa ya kuwekeza katika elimu kwa kujenga shule ili kuwajengea maadili ya kiroho na kijamii yatakayowasiaia kuwa na hofu ya Mungu na kukua katika maadili memandani ya jamii. 

“Wakati Dunia inawaya waya kama mlevi watoto wanajikita kwenye ulevi,uvutaji bangi sisi tujikite kuwarudhisha njia sahihi  taasisi ya elimu inamjenga mtoto tangu akiwa mdogo akili yake haijachafuliwa taasisi ya elimu inalipa sana inawez kubadili maisha ya mtoto ndani ya muda mfupi tuinuke tufanye kazi”,alishauri Mkurugenzi.


Post a Comment

0 Comments