HALMASHAURI YA MPWAPWA YATOA PONGEZI KWA ASASI ZA KIRAIA.



📌NOEL STEPHEN 

UONGOZI wa Halmashauri ya Mpwapwa  mkoani Dodoma umeyapongeza mashirika yasiyo kuwa ya kiserikali katika jitahada walizoezionyesha katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa COVID 19.

Pongezi hizo zilitolewa na kaimu Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo  bwana Komlo Njovu katika kikao  za Wadau wa mashirika yasiyo kuwa ya kiserikali katika kujadili changamoto za ulinzi wa utu wa mtoto na mwanamke. 

Njovu amesema bila kujali afua mbalimbali zinazofanywa na mashirika hayo wilayani hapa lakini kipindi cha ugonjwa wa COVID 19 mashirika waliunganisha Nguvu za Pamoja katika kutoa elimu, Kagawa vifaa na dawa za kujikinga na ugonjwa huo. 

Aidha Bwana Njovu amesema kuwa nguvu zilizo tumika katika mapambano ya ugonjwa huo amezitaka tasisi hizo kutumia Nguvu hizo katika kupambana na magonjwa mengine ya mlipuko Kama kipindu pindu,Kuharadamu, Kimeta na magonjwa mengine mengi. 

"Tulifanikiwa sana katika mapambano ya COVID 19kwa sababu tuliunganisha nguvu za pamoja sasa ninawaomba nguvu na mbinu zile zile zitumike katika mapambano ya magonjwa mengine ya mlipuko ili jamii unufaike na iishi bila magonjwa "aliongea. 

Hata hivyo bwana Njovu amedai kuwa mbali na magonjwa hayo pia zipo changamoto nyingi zinazo ikabili jamii yetu Kama ukatili wa kinjisia, mimba mashuleni ,na changamoto za umaskini wa wa kipato kwa jamii.

Kwa upande wake mganga mfawidhi wa wilaya ya Mpwapwa Dkt Hamza Mkingule amesema magonjwa ya mlipuko ni magonjwa ambayo hutokea kwa muda fulani na kuisha ghafla lakini ni magonjwa ambayo huweza kuuwa idadi kubwa ya watu Kama udhibiti huakufanyika kwa makini. 

Dkt Mkingule amedai kuwa  endapo jamii ikizingatia kanuni za afya na maelekezo ya wataalam wanakuwa kwenye upande salama kuto kukubwa na magonjwa hayo. 

Pia amesema kuwa kuna baadhi ya magonjwa ya mlipuko hutokea kutokana na uzembe wa jamii kushidwa kutimiza masharti ya kanuni za afya Kama kuto kuwa na vyoo na hivyo kujisaidia vichakani na hivyo husababisha kipindu pindu.

Amedai kwa Mpwapwa miezi ya kumi na mbili ni miezi ambayo wilaya inakuwa kwenye hatari kubwa ya kukubwa na magonjwa ya mlipuko kutokana na kuwa msimu wa mvua  na kipindi cha matunda mengi hivyo wananchi kushidwa kudhibiti uchafu na hivyo kutishia kutokea kwa magonjwa hayo ya mlipuko. 

Mmoja wa washiriki wa kikao hicho mwakilishi wa kundi la walemavu Bwana Kandido Mnemele alisema kuwa kipindi cha ugonjwa wa COVID 19 kundi la walemavu waliachwa nyuma kutokana na miundo mbinu yao kuto kuwa rafiki katika maeneo mengi ya tasisi za serikali. 

"Ukweli tunashukuru serikali na Wadau lakini pamoja na jitihada hizi je kundi la watu wenye ulemavu walifikiliwa, watu wasio sikia,  na walemavu wa viungo waliwekewaje mazingira ya kujikinga na maradhi hayo na walemavu wa kusikia walifikiwaje na elimu bila kuwapo mkalimani wa Lugha ya alama? Aliohoji Kandido. 

Akijibu hoja hizo kaimu afisa utumishi wa halmashauri ya Mpwapwa Bi Kibibi Edward alikili kuto kuwapo kwa mkalimani wa Lugha ya alama katika halmashauri yake na alisema kwa mtumishi yoyote atakae taka Kwenda kusomea Lugha ya alama atapewa kipaumbele. 

Pia amesema COVID 19 iliwafundisha mengi ikiwamo kushirika kila makundi katika mapambano ya magonjwa yote ya mlipuko ili kuweza kufikia ufanisi wa haraka. 

MWISHO. 

Post a Comment

0 Comments