📌Na Saleh Ramadhan.
"Ng'ombe aina ya mpwapwa ni Tunu ya Taifa maana ng'ombe huyu ni matokeo ya utafiti uliolenga kuzalisha ng'ombe chotara kwa ajili ya nyama na maziwa kwa wingi katika mazingira kame" amesema Dr. Aluna chawala.
"Halmashauri zote zenye wafugaji wengi zikifanya utaratibu wa kufikisha elimu ya teknolojia hii ngazi ya kijiji mpaka kata itawafanya wafugaji wavutiwe na ufugaji huu". Amesema Deogratius masao.
Naye Mtafiti idara ya mbuzi Boniface paschal amebainisha kuwa mbuzi aina ya malya au Blended ni mbuzi aliyetokana na utafiti uliokusudia kuzalisha mbuzi anayefaa kwa nyama na maziwa.
" utafiti huu wa mbuzi aina ya malya ni kumuongezea lishe na kipato mfugaji, mbuzi huyu ni mchanganyiko wa mbuzi Asili-kamorai kutoka pakistani na Boer kutoka Africa Kusini, pia wanauwezo wa kuzaa watoto mapacha au watatu na wanauwezo wa kuzaa hadi Mara 3 katika kipindi cha miaka miwili" amesema
Serikali kupitia Tume ya Taifa ya
sayansi na Teknolojia (COSTECH) imetumia Billion 50 katika kufadhili Miradi ya
utafiti na ubunifu nchini ambapo Miradi zaidi ya 100 imefadhiliwa na Asilimia
70% imekamilika.
Mwisho.
0 Comments