📌NOEL STEPHEN
UGONJWA wa COVID 19 ni ugonjwa wa kuambukizwa ambao unatajwa kuwa miongoni
mwa magonjwa ya mlipuko unaosababishwa
na virus vya corana.
Virusi hivyo vipya
havikuwa vikafamika hapo awali
na sayansi ya tiba , Corona ni kirusi
kinachosababisha maradhi kwa wanayama na bidamau pia hasa kwa kushambulia katika njia ya hewa na
mfumo wa upumuaji .
Mara baada ya Waziri
waziri wa Afya Mhe Ummy Mwalimu
kumtangaza mgonjwa wa kwanza wa ugonjwa
wa COVID 19 mnamo mwezi Maachi mwaka huu
,jamii ilianza kupata shaka na kuingiwa
na wasiwasi na hofu kubwa juu ya kuweza
kuukabili ugonjwa huu.
Kufuatia hali hiyo Serikali kupitia waziri mkuu Mhe Kasim
Majaliwa alikuja na tamko juu ya kujikinga na
ugonjwa huo ikiwemo kunawa mikono,
kutumia barakoa katika sehemu zote za mikusanyiko na katika sehemu za huduma kama hospitalini shuleni , mahakamani na sehemu zingine zote
ikiwemo kutenga maeneo ya kuwahifadhi waliokwisha ambukizwa ugonjwa huo(karantini).
Aidha Waziri Mkuu
alitangaza kufugwa kwa shule zote za seikali na binafsi kwa kipindi cha mwezi mmoja kuanzia Machi
17 2020 .
Baada ya tangazo hilo kutoka kwa Serikali,swali kubwa
lilikuwa ni juu ya mustakabari wa elimu hususani kwa wanafunzi waliokuwa kwenye
madarasa ya mtihani.
Serikali kwa kushirikiana na wadau wa elimu walijifungia
kuumizwa kichwa na wakaja na jibu la namna bora ya wanafunzi kuendelea na
masomo katika kipindi ambacho nchini ipo kwenye mapambano dhidi ya ugonjwa huo.
Na jawabu likawa moja
tu; wanafunzi kufuatilia vipindi vya masomo
kwa kutumia vyombo vya habari kama radio ,luninga na simu mfumo huo ambao ulikuwa rafiki kwa wanafunzi wa
mijini na wanao miliki vyombo hivyo.
Hii ni hatua njema kabisa katika ukombozi wa elimu katika
kipindi kigumu cha mpito,lakini swali kubwa likawa je;njia hiyo ilikuwa msaada
kwa wanafunzi wote nchini?
Ester Mwahisi mkazi
wa Kata ya Mazae katika Wilaya ya Mpwapa
anasema kuwa kutokana familia yake
kushidwa kumiliki simu ambayo inaweza Kutumia mtandao na kutokuwa na Runinga
wala radio watoto wake hawakuweza wake kufuatilia vipindi hivyo.
Hali ya kipato kwa baadhi ya wazazi katika maeneo mbalimbali nchini kiliwanyima
fursa baadhi ya wanafunzi kupata elimu
hiyo ambayo ilikuwa inatolewa katika muda sawa na ule wa shule.
Kwa upande wake Charles Jonson ambaye ni Mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Idilo iliyop
Wilaya ya Mpwapwa amesem kufungwa kwa shule katika kipindi cha Corona kuliwaathiri wanafunzi katika maeneo hayo ya vijijini hususani wale
waliokuwa kwenye madarasa ya mitihani wakiwemo darasa la Nne na darasa la Saba.
Tulipo fungua tu tulijaribu kuwaliuza wanafunzi wangapi walikuwa wanafuatilia masomo kwa njia ya televisheni kati ya wanafunzi 48 ni wanafunzi 7 tu ndio walikuwawakifuatilia lakini nao sio hadi mwisho walifuatilia mwanzoni tu baadae wakaacha kufuatilia.
Charles Jonson
Jonson amesema mara walipofungua shule tu waliandika mtihani
wakujipima ambapo amesema hakuna mwanafunzi aliye pata daraja la kwanza.Amesema
lengo la mtihiani huo ni kupima wanafunzi hao kama wanakumbuka chochote
walichofundishwa katika kipindi hicho walipokuwa kwenye mapumziko ya lazima.
Mwalimu Jonson amesema ni wanafunzi wachache
tu ndio walipata alama B na wengi
walipata alama C wakati kabla shule hazijafungwa Hapo tarehe 17 Machi watoto
wengi walikuwa kwenye daraja A hivyo walitoa mtihani huo ili kuweza kujua
waanzie wapi kuziba mapengo ufundishaji na ujifunzaji kwa wanafunzi wa shule
hiyo.
Kwa upande wake Mery Chakupewa afisa Elimu Msingi Wilaya ya Mpwapwa amekiri kuwa mfumo wa usomaji
kwa kwa njia ya mitandao imewasaidia baadhi ya watoto na hivyo haikuweza
kuwadaidia watoto wote hasa waishio vijijini.
Mwl.Chakupewa amesema serikali kupitia wizara husika ya Uchukuzi na Mawasiliano lazima iweze
kuboresha mifumo hiyo kipindi kingine kama likitokea janga kama la CORONA
linaloweza kusababisha shule kufungwa kuweza kuwajumuisha hata Watoto wa
vijini.
Amesema japo kuwa serikali imefanya kazi kubwa kajaribu
kusambaza umeme katika vijiji vingi hapa nchini kwa kupitia mradi wa Wakala waUmeme
vijijini (REA) lakini baadhi familia zimeshidwa kuunganishaa umeme huo kwenye
nyumba zao ili kuweza kunufaika na fursa za Serikali kama hizo kutokana na uduni
wa maisha yao.
Aidha amedai kuwa pia
kuna wakati wa kipindi cha CORONA baadhi ya Wazazi walikuwa wakiwatumia Watoto
hao katikati kazi mbali mbali kama za kuuza biashara ndogo ndogo hivyo
ulikosekana muda wa kusoma kwa watoto hao.
Wakati watoto wengine wakiwa kwenye runinga wakijifunza,wazazi wengine walitumia muda huo kutumikisha watoto wao kuwasaidia kuuza biashara zao.
Mery Chakupewa
Naye mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Jabir Shekimweri amesema
katikati kipindi cha likizo ya Corona kama wilaya kupitia Idara husika waliweza
kutoa maelekezo na Elimu kupitia makanisani na misikitini namna bora ya Wazazi
kuwasaidia Watoto wao kujifunza wakati
wa kipindi hicho cha mpito.
Bila Shaka madhara lazima yawepo kutokana na mwamko mdogo Wa baadhi ya wazazi, lakini umaskini wa kipato kwa baadhi ya familia hivyo haikwepeki
Jabir Shekimweri
0 Comments