📌NA HAMIDA RAMADHANI.
WAGANGA Wakuu wa Mikoa na Halmashauri kote nchini wameagizwa kuacha kukaa maofisini na badala yake wametakiwa kutoka na kwenda hospitali kuchukua na kujua maoni ya wananchi wanokwenda kupata huduma katika hspital husika.
Akiongea na wafanyakazi wa Hospital ya Rufaa ya General pamoja na wagonjwa,Gwajima amesema waganga wakuu wa Mikoa na halmashauri wahakikishe wanajiwekea utaratibu wa kuchukua maoni ya wanainichi kwa kila hospital husika.
Aidha kwa Upande mwingine amewataka wananchi wanapatiwa matibabu hospitalini hapo wahakikishe wanatoa maoni yao kama huduma waliopata ni zuri au mbaya kupitia namba za simu husika na Sanduku la maoni.
" Wananchi msiwe waoga kutoa taarifa au kueleza kero mnazokumbana nazo pindi mnapokuja kuchukua huduma hosptalini kunamasanduku ya maoni pelekeni mule maoni yenu msiondoke na dukuduku moyoni mwishoe tukute malalamika yenu kwenye mitandao ya kijamii," amesema Dkt Gwajima.
DAWA
Kwa Upande wa dawa serikali imekuwa ikitenga bajeti ya fedha lakini suala la dawa Iimekuwa ni changamoto kila kona kutokana na kutokuwa na Takwimu za uhakika za dawa .
" Sasa kutokana na hayo naagiza ndani ya siki 10 kuwe na mabadiliko hospitalini hapa na dawa zote ziwekwe kwenye mfumo wa kompyuta
Kwa Upande wao wananchi waliofika kupata huduma ya matibabu hospitalini hapo walipongeza utaratibu nzima wa huduma wanapotiwa katika hospitali hiyo huku wakikiri mbele ya Waziri huyo kupatiwa huduma safi bila manyanyaso.
Akiongea kwa niaba ya wananchi wenzake Andrew Thomas Mkazi wa Chisichili uliopo nje kidogo na Jiji la Dodoma Mkonze amesema huduma wanapatiwa vizuri tena kwa wakati.
Hata hivyo amemuomba Waziri wa Afya kuwaboreshea sehemu ya kusubiria wagonjwa kwani sio rafiki na wamekuwa wakifukuzwa na walinzi wakidai kuwa hawaruhusiwi kulala.
Akijibu kero Waziri wa
Afya Dkt Gwajima ameagiza hospitali hiyo kuhakikisha mkandarasi anakuja
mara moja kutathimini ujenzi wa sehemu maalumu pa kusubiria
wagonjwa uanze mara moja.
0 Comments