Lakini je, tuache kuchukua njia sahihi kwa sababu ya ukosefu wa uelewa juu ya swala hili? Kilimo cha malisho ndio njia pekee ya kupambana na mabadiliko ya tabia ya nchi na kusaidia ufugaji wa kisasa kwa mategemeo ya kupata bidhaa bora.
Uhakika wa malisho ni njia itakayomwezesha na kumuhakikishia mfugaji uhakika wa chakula cha mifugo wakati wa kiangazi ambapo Mfugaji mwenye kuweza kudhubutu kulima malisho atakuwa na uwezo wa kuvuna na kuweka akiba ya malisho(kipindi cha msimu wa masika) na kutumia akiba hiyo kipindi cha kiangazi wakati ambapo kuna upungufu mkubwa wa malisho.
Jukumu hili linabaki kwenye mamlaka husika kuhakikisha mbegu za malisho bora zinapatikana ili elimu ya kilimo malisho iambatane na mbegu za malisho.
Hata hivyo katika kipindi ambacho mifugo mingi inakufa tusiwalaumu wafugaji kwa kuwaambia hawataki kuuza mifugo haswa msimu wa kiangazi wakati tunajua mapungufu ya soko letu la mifugo na mazao yake na wala hatupaswi kuwalaumu kutangatanga wakati tunajua hali ya machunga hapa nchini.
Tunachotakiwa
kufanya,ni kukomboa ufugaji na ukaendelea kushamiri kwa wafugaji hawa hawa
tunaowalaumu kwa kuhamasisha kilimo cha malisho kwa wafugaji na kutumia
mashamba darasa kuelimishia wafugaji hakika kilio cha malisho msimu wa kiangazi
tutakitokomeza.
Na kwa kuwa wafugaji
wengi wa kitanzania ni wale wenye shughuli asili ambazo kwa namna moja au
nyingine huchochea uharibufu wa mazingira kutokana na kuhama hama,ufugaji huu
wa kisasa utasaidi kuondoa migogoro mingi ya ardhi.
Lakini kama ufugaji ndio utamaduni wao je, ni kweli tuna sababu ya kupoteza utamaduni huo? Jibu ni hapana,bali tunacho takiwa kufanya ni kusaidia kuboresha mfumo wa ufugaji kuhakikisha kuwa mfugaji anafaidika na ufugaji wake wa kila siku kwa ajili ya kuongeza kipato na kustawisha uchumi wa nchi.
Kwa umuhimu
huo,Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Tume ya
Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) katika kipindi cha miaka 10
(2010-2020) imewezesha miradi 100 ya utafiti na ubunifu ambayo inaendelea
kuwanufaisha watanzania katika kuwaongezea kipato kwa kutoa Bilioni 50 .
Malisho ni chakula muhimu sana kwa mifugo, kwa kawaida mifugo hupata chakula hasa nyasi katika malisho ya asili,lakini chakula hiki hakitoshelezi mahitaji kwa kuwa hakina viinilishe vya kutosha kwa afya bora ya mifugo Kwa mfano, kiasi cha protini na madini ni kidogo ukilinganisha na malisho ya kisasa,amesema Fupi
Fupi ameongeza
kuwa,mambo makuu mawili kwa mfugaji wa kitanzania yanayomkuba ni mabadiliko ya
tabia nchi linalotokana na ongezeko kubwa la watu ambalo linazidi kuimega ardhi
ya malisho kwa shughuli mbalimbali kama makazi na kilimo.
“Serikali imezidi kujitahidi kumaliza migogoro hii lakini imekuwa ikijirudia kwa sababu hakuna suluhisho la mahitaji ya mfugaji katika eneo lake kutokana na wafugaji wengi kutokuwa na uelewa wa malisho ya kisasa,’’anasisitiza.
Mtaalamu huyo anaeleza
kuwa asilimia 60 ya eneo la ardhi hapa nchini ni mbuga za malisho ya asili
ambayo hutegemewa kwa chakula na mamilioni ya mifugo na wanyama pori walakini
malisho haya hukomaa na kukauka mapema zaidi na hivyo kusababisha lishe yake kuwa
duni na ustawi hafifu kwa wanyama wanaoyatumia hususani nyakati za kiangazi .
Dk.Mwalingo anasema kutokana na upungufu wa ubora wa malisho haya, upo umuhimu wa kuotesha aina bora za malisho kwa kuzingatia Utayarishaji wa shamba, Kurutubisha ardhi na upandaji.
“Mkulima
anapaswa kuhakikisha amepiga harrow ili kulainisha udongo kurahisisha
uotaji wa mbegu za malisho ambazo nyingi huwa na umbo dogo,kurutubisha ardhi ni
muhimu ili kurekebisha upungufu wa madini mbalimbali yanayohitajika na
mimea,”anasema.
Hata hivyo Mwalongo
anasema ubora wa mbegu unapaswa kuzingatiwa kutokana na sehemu zinazoaminika
kama vile Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Mabuki, vituo vya Utafiti wa Malisho ya
Mifugo kama Kongwa na Mpwapwa (Dodoma).
Mbegu hizi ziliunganishwa kati ya majani ya asili na mbegu kutoka Austrelia ambayo ina virutubisho vingi ambavyo licha ya kuhifadhi mazingira wanyama wengi pia wanaipenda.
..................
0 Comments