📌 Na RAMADHAN HASSAN
CHUO
Kikuu cha St John kilichopo Jijini Dodoma kimeanza kutumia mfumo wa kufundisha
kidigital maarufu (E learning) ambapo mfumo huo umeonesha mafanikio
makubwa.
Hayo
yameelezwa na Makamu Mkuu wa Chuo hicho.Profesa Yohana Msanjila wakati akizungumza katika mahafali ya 11 ya chuo
hicho.
Katika
mahafali hayo,chuo hicho kimewatunuku Shahada mbalimbali jumla ya
wahitimu 1322 ambapo kati yao wahitimu 631 ni wa kike sawa na asilimia 47.7 ya
wahitimui wote na wanaume ni 691 sawa na asilimia 52.3.
Profesa
Msanjila amesema katika mahafali ya mwaka jana chuo kilieleza azma yake
kukibadilisha na kutumia mfumo wa kidigitali ambapo amedai mpango huo ulilenga
kuwekeza zaidi katika mifumo ya Tehama ili kuweza kutoa mafunzo kwa wanafunzi
kwa njia ya kisasa zaidi.
“Napenda
kuifahamisha hadhara hii kuwa mpango wetu unakwenda vizuri katibu wahadhiri
wote wamepatiwa mafunzo kwa nyakati tofauti mafunzo hayo yamewezesha kozi
nane.
“Kupitia
‘moodle’ wahadhiri na wanafunzi sasa wanakutana mtandaoni na
kufanya mambo yote yanayotakiwa kufanyika katika ufundishaji na
ujifunzaji wa darasa la kawaida hii ni kuesema kuwa mwalimu anaweza
kufundisha,kutoa majaribio,kutoa mitihani kusahihisha na kutoa matokeo humo
humo mtandaoni,”amesema.
Amesema
mpango wa kufundisha kidigital unaenda sambamba na mpango wa
kuimarisha utumiaji wa E-Library kwa ajili ya kuwezesha wanafunzi na
wafanyakazi waweze kusoma vitabu na nyaraka mbalimbali muhimu
hupitia online.
“Ili
kufanikisha mpango huo chuo kimeongeza uwezo wa bandwidth kutoka mb 20 hadi
kufikia 40 ili kuwezesha wanafunzi na walimu kusoma kwa wepesi,”amesema.
Amesema
chuo kinaendelea na mchakato wa kumalizia kuandaa program mpya ya BSc in IT
ambayo itakuwa ni kichocheo cha kutumia mbinu za kidijitali.
Kwa
upande wake,Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo hicho,Profesa Penina Mlama amesema
katika mwaka huu wa fedha chuo kimepanga jengo la utawala ambapo amedai ujenzi
huo unalenga kuongeza idadi ya ofisi kwa wafanyakazi wake kutokana na ongezeko
la wanataaluma.
“Hivi sasa tuna uhaba wa Ofisi kwa wafanyakazi wetu jambo linalofanya wafanyakazi kushirikiana kukaa ofisi moja,kukamilika kwa jengo hilo kutapunguza tatizo la uhaba wa ofisi kwa wafanyakazi wetu,”alisema.
Kwa upande wake,Mkuu wa Chuo hicho,Askofu Mkuu Mstaafu,Donald Mtetemela amesema chuo kinafanya kila kiwezavyo kuendeleza mahusiano ya kitaaluma na vyuo mbalimbali ndani na nje ya nchi.
Amevitaja vyuo hivyo kuwa ni pamoja na Kenyatta University University of London,Norwegian na Danish Institute for international studies.
0 Comments