📌Na
Ramadhan Hassan
MKURUGENZI
wa michezo nchini,Yusuph Singo ameliagiza Baraza la Michezo Nchini (BMT)
kuwaondoa madarakani viongozi wa vyama
vya michezo wanaong'ang'ania madaraka bila kufuata Katiba.
Akizungumza leo Jijini Dodoma katika Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC),Mkurugenzi huyo wa michezo amesema Serikali imeanza kutafsiri kwa vitendo kauli ya Rais,Dkt.John Magufuli ya kutaka sekta ya michezo kuboreshwa.
Mkutano huo ulihudhuriwa na viongozi wa vyama vyote vya michezo nchini,pamoja na baadhi ya wanamichezo waliowahi kufanya vizuri na kushiriki mashindano mbalimbali ya kimataifa.
"Nawaagiza
BMT mzaha sasa umepitwa na wakati viongozi hawataki kuondoka muwaondoe,nendeni
vizuri,viongozi ambao hamtaki vyama ni kwa niaba ya Watanzania tu.
Tunatarajia kutoka sehemu moja kwenda nyingine Tennis nawapongeza Sana hatutaki kusikia mnalalamikiana
Yusuph Singo.
Pia,amevitaka
vyama hivyo kuhakikisha vinaendeleza michezo kama ilani ya uchaguzi ya BMT inavyotaka.
"Sasa
Mheshimiwa Rais anasema Watanzania wanataka ushindi,ndugu zangu tuhakikishe
tunaendeleza michezo hata ilani ya uchaguzi inalizungumzia hilo.
"Sisi
kama Serikali tumeanza kutafsiri maelekeazo ya Rais na nyie viongozi nendeni
mkatafsiri mazoea yamekwisha,hamuheshimu hata Katiba zenu,ninaomba kila mmoja
wenu mtakaporudi jipangeni,"amesema.
Katika
hatua nyingine,amesema Desemba 19 mwaka huu,Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na
Michezo,Innocent Bashungwa anatarajia kukutana na wadau wa michezo vikiwemo
vyama vya michezo kumzungumzia mpango wa Taifa wa michezo.
Hivyo
amevitaka vyama hivyo kupeleka viongozi sahihi na sio kutuma Wawakilishi.
"Hili
ni very serious nitakuwa na mkutano Tarehe 19 kutakuwa na mkutano wa wadau
tunaongelea mpango wa Taifa wa kuendeleza michezo,nawaomba mje,msitume
wawakilishi,"amesema.
Mwisho
0 Comments