Makamu mwenyekiti wa tume ya haki za binadamu
na utawala bora akitoa tamko kwa waandishi wa habari
📌NA PENDO MANGALA
TUME ya Haki za Binadamu na utawala bora nchini imesema kuwa licha ya kuwepo
kwa jitihada mbalimbali za kupinga ukatili wa kijinsia lakini bado kuna
changamoto ambazo zinakwamisha utekelezaji wa majukumu ya Serikali katika
kujenga jamii salama isiyo na vitendo vya ukatili wa Kijinsia.
Hayo yameelezwa leo Jijini Dodoma na Makumu Mwenyekiti wa Tume
hiyo,Mohamed Hamis Hamad wakati akitoa tamko kwa waandishi wa habari kuhusu
maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa Kijinsia Duniani ambapo amezitaja
baadhi ya changamoto hizo kuwa ni pamoja na mila na desturi pamoja naimani
zinazohusu watoto wa kike kuolewa katika umri mdogo badala ya kuendelea na
masomo.
Aidha amesema kuwa kumekuwepo na mila za ukeketaji watoto
wa kike pamoja na rushwa ya ngono katika maeneo ya kazi na Vyuo Vikuu ni kikwazo
katika kufanikisha juhudi hizo za Serikali.
Kutokana na hayo Tume ya Haki za Binadamu na utawala bora
inaisisihi Jamii kuacha mila ,imani na desturi potofu ambazo ni chachu ya
kukithiri kwa matukio ya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto.
“Tume inatoa msisitizo kwa watumishi wa Umma na Mashirika yasiyo
ya Kiserikali kuzingatia na kuheshimu kanuni na taratibu za maadili ya utumishi
wa Umma ili kuondokana na vitendo vya ukatili wa kjinsia dhidi ya wanawake na
watoto”,alisema.
Sambamba na hilo Makamu huyo,aliwataka wananchi kutofumbia macho
matukio kama hayo yanapotokea katika jamii kwa kutoa taarifa kwawakati katika
Mamlaka husika ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa.
Katika hatua nyingine ameipongeza Serikali kwa jitihada
mbalimbali zilizochukuliwa katika kukabiliana na vitendo vya ukatili wa
kijinjsia nchini ambapo miongoni mwa jitihada hizo ni pamoja na kuanzisha
mipango mikakati ya kutokomeza ukatili wakijinsia dhidi ya wanawake na watoto
Tanzania bara na Zanzibar
“Mipango hii imelenga kupunguza ukatili wa kijinsia kwa kiasi
kikubwa huku kukiwepo na madwati ya Jinsia na watoto katika Vituo vyaPolisi
ambapo jumla ya madawati 420 yameanzishwa ambapo yamewezesha wahanga 58,059
kufikiwa na kupatiwa huduma.”Alisema
Kwa Upande wake Kamishna wa Tume hiyo,Fatma Rashid Khalfan
amesema wao kama Tume watatoa uwezeshaji kwa Wanavyuo ambao walifanya tafiti
kuhusiana na ukatili wa kijinsia kwa kuandaa makongamano kupitia klabu
mbalimbali ili kuweza kutokomeza vitendo hivyo
Kampeni hii ya kimataifa inayojulikana zaidi kwa jina lasiku16
za kupinga ukatili wa kijinsia huadhimishwa kila mwaka kuanzia tarehe25 Novemba
na kufikia kilele Disemba 10 ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni “Tupinge ukatili
wa kijinsia mabdailiko yanaanza na mimi”,
MWISHO
0 Comments