📌 HAMIDA RAMADHANI
MKURUGENZI wa Sera na Mipango Wizara ya Afya Edward Mbanga amesema asilimia 60 ya watanzania hutumia huduma ya Tiba asili kwa kujificha wakidhani kwamba tiba hiyo ni uchawi.
Amezungumza hayo leo jijini hapa wakati akimuwakilishi Katibu Mkuu Wizara ya Afya katika Mkutano uliowakusanya wadau wa Tiba asili kutoka maeneo tofauti tofauti hapa nchini.
"Tunatakiwa kujiuliza swali kama wadau wa tiba asili ni kwà nini watanzania hawajivunii wala kujitangaza juu ya umuhimu wa huduma hii ya Tiba asili wakati Takwimu zinaonesha idadi kubwa ya watumiaji wa Tiba hii mbadala hapa nchini," amesema Mkurugenzi Mbanga.
Na kuongeza kusema kuwa " Tiba asili sio kitu cha ajabu wala sio uchawi au ramli , tuachane na ukoloni uliojengeka vichwani mwetu utakuta mtu akijitambulisha mganga wa tiba asili mtu huyo atachekwa kweli tena sio kicheko tu cha kawaida ni kicheko cha kubezwa," Amesema.
Aidha amewataka wadau hao kukubaliana na kujiuliza nini kifanyike, tumefika wapi ,tuko wapi, na tutafikaje huko tunapotaka kwenda katika kukuza na kuitambulisha tiba asili hapa nchini.
Amesema licha ya Tafiti za tiba asili kufanyika tangia mwaka 1969 lakini mpaka Sasa haujaonesha tumenufaikaje kama Taifa.
"Sasa nyinyi ni wadau muhimu wa tiba asili mkikubaliana na kuwa kitu kimoja katika kuitangaza tiba asili nchini na kote duniani basi tutaweza kumaliza changamoto zilizopo na kufanikiwa kuwaachia au kurithisha thamani vizazi vyetu vijavyo," amesema.
Na kuongeza kusema kuwa
Mpango wa serikali ni kuanzisha vituo vya tiba asili katika Kila ngazi ya Kijiji, Kata Tarafa na Halmashauri zote na suala hili la kuanzisha vituo vya tiba mbadala tunaweza kuwa kama vivutio hivyo itatusaidia kujipanga kihistoria zaidi
Hata hivyo amesema kabala ya kuja wakoloni tulikuwa tunasayansi yetu ambapo tulikuwa tukitumia tiba asili kujitibu pindi tulipokuwa tunaumwa sasa ni wakati muwafaka wa kurudisha sayansi yetu na tuachane na sayansi ya kikoloni.
"Tanzania tuna miti ,dawa ya kutosha na imekuwa ikitunufaisha kama Taifa, hivyo basi ili kuifikisha nchi hii kufika zilipofika nchi zingine tumekutana hapa kujadili nini kifanyike na tunaanzia hapa kama Takwimu zinaonesha asilimia 80 ya dawa tunaagiza kutoka nje ya nchi ni kwanini tusianzishe viwanda vya kutengeneza dawa hizo uwezo huo tunao na ndio maana tumekutana," amesema Mbanga.
Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Tiba na huduma za Afya kutoka Wizara ya Afya Dkt Grace Magembe amesema awali tiba asili ilikuwa haina msukumo wala kujulikana na umekuja kujulikana kipindi cha corona.
Naendapo tungeweka msukumo na mkazo katika kuitambulisha tiba asili tungefanikiwa kukuza uchumi wa nchi yetu
Dkt Magembe
0 Comments