AGIZO LA MKUU WA WILAYA YA MPWAPWA MH:JABIR SHEKIMWERI KWA MKURUGENZI HILI HAPA.

 

📌BARNABAS KISENGI

MKUU wa wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma JABIR SHEKIMWERI amemwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halimashauri ya Wilaya ya Mpwapwa kuhakikisha mwezi huu wanamaliza kutengeza madawati ya shule za secondary na msingi ili ifikapo January 2021 wakati wanafunzi wa kidato cha kwanza na darasa la kwanza wanapoingia darasani kusitokee mwanafunzi at a Kaye kaa chini akiwa darasani. 

Kauli hiyo ameitoa wakati wa kikao cha watendaji wa halmashauri na wakuu wa idara wa halimashauri hiyo kwa kujiwekea mikakati ya utendaji kazi wa mwaka 2021 wilayani hapo. 

Nakuagiza Mkulugenzi Mtendaji na timu ya wasaidizi wako wa idara ya elimu yani afisa elimu secondary na msingi ifikapo January 2021 wakati shule zinafunguliwa nisije nikasikia Kuna mwanafunzi yoyote anakaa chini kwa kukosa dawati hata moja.

DC Shekimweri

Shekimweri amesema kuwa hakuna sababu ya mwanafunzi kukaa chini kutokana na serikali kutoa pesa na wilaya sasa ina kiwanda cha kutengeneza madawati hivyo watendaji wawajibike kila moja kwenye eneo lake na maafisa elimu wote washakikishe wanasimamia kuhakikisha madawati yanakamilika kwa wakati na kusambazwa katika shule zote zenye upungufu wa madawati kabla ya shule kufunguliwa mwakani sanjari na kuhakikisha wanamalizia na ujenzi wa maboma ya vyumba vya madarasa wilayani hapo mapema.

Aidha amewataka wazazi wote ambao watoto wao wamefaulu kuhakikisha katika kipindi hichi cha mwezi December wanawaanda watoto wao kwa kuwaandalia Sare za shule,madaftari na viatu kwakuwa mzigo mzito wa Ada tayari serikali umekwisha ubeba, hivyo wazazi na walezi wawajibike kwa upande wa mambo yanayowahusu watoto wao na kwa mtoto ambaye muda wa kuripoti shuleni mzazi atakayemficha mtoto wakae wajue serikali haijalala na inamacho makali hivyo wazazi watakao husika watachukuliwa hatua Kali za kisheria wilayani hapo. 

 

Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa halimashauri hiyo Paulo Sweya amemhakikishia Mkuu wa Wilaya kuwa maagizo hayo yote watayafanyia kazi kwa kushirikiana Kama timu na maafisa elimu na wakuu wa idara wote kwa kuunda kikosi kazi ili kuhakikisha swala la madawati linakwisha katika wilaya hiyo. 

"Nikuhakikishie mkuu wa wilaya maelekezo yako tunayafanyia kazi na mimi Kama Mkulugenzi ambaye ndiye msimamizi mkuu wa shughuli za halimashauri nilishaunda timu yangu ya wakuu wa idara kusimamia utengenezaji wa madawati na umaliziaji wa maboma ya vyumba vya madarasa na serikali ilishatoa fedha hivyo ni jukumu letu kuhakikisha tunatekeleza wajibu wetu kwa kila mtumishi wa idara"amesema Sweya

Shekimweri pia ametumia nafasi hiyo kuipongeza serikali ya awamu ya tano na kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Magufuli kwa ushindi mkubwa alioupata mwezi Oktoba wa kushinda kwa kishindo kuongoza tena kwa kipindi cha pili.

Post a Comment

0 Comments