📌ANGELA MSIMBIRA
OR-TAMISEMI
Waziri Mkuu wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Mjaliwa (Mb) ametoa siku
15 kwa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino, Wakala wa Majengo Tanzania
(TBA) na Suma JKT kuhakikisha ujenzi wa Hospitali ya
Uhuru unakamilika ifikapo disemba 5, 2020.
Akikagua maendeleo ya
ujenzi wa Hospitali hiyo leo Jijini Dodoma Mhe. Majaliwa amesema Hospitali ya
Uhuru ni moja kati ya miradi ya kimkakati ya Serikali ya Awamu ya Tano ya
kuimarisha utoaji huduma katika Sekta ya afya ambayo inaanzia
kuboresha kuanzia ngazi ya zahanati, vituo vya Afya, Hospitali za Wilaya,
Hospitali za Rufaa na Hospitali za Magonjwa makubwa.
Anaendelea kufafanua kuwa Serikali imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha inaboresha huduma za afya kwa lengo la kutoa huduma bora kwa wananchi, hivyo imejikita katika kuhakikisha miradi yote ya kimakakati inakamilika kwa wakati ili ianze kutumika
Halmashauri ya Wilaya
ya Chamwino, Wakala wa majengo (TBA), Suma JKT, hakikisheni ujenzi wa
Hospitali hii unakamilika kwa wakati, fanyeni kazi usiku na mchana, jengeni
vibanda na kuhamia kwenye eneo la ujenzi, ongezeni wafanyakazi ili
kukamilisha ujenzi kwa wakati uliopangwa
Mhe. Majaliwa
Mhe. Majaliwa amesema
miradi ya Kimakakati inatakiwa ikamilike kwa wakati na Watanzania wanahamu ya
kuona miradi inakamilika na kuanza kutoa huduma hivyo fanyeni kazi kwa
weledi ili kuweza kukamilisha ujenzi wa Hospitali hiyo muhimu kwa jamiiWaziri
Mkuu atoa siku 15 kukamilika kwa Hospitali ya Uhuru
Akitoa taarifa ya
maendeleo ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Chamwino, Katibu Mkuu Ofisi ya
Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhandisi Joseph Nyamhanga amesema
ujenzi wa Hospitali ya Uhuru imekadiriwa kutumia zaidi ya shilingi bilioni
3.995 na kiasi kilichotengwa ni shilingi bilioni 3.410 ambapo zaidi ya
shilingi milioni 995 zilikuwa ni fedha za maadhimisho ya siku ya uhuru wa
Tanganyika na shilingi bilioni 2.415 ni gawio la kampuni ya simu ya
Airtel.
Naye Msaidizi wa Mkuu wa
JKT Colonel Laurence Angelo Lupenge amesema mradi wa ujenzi wa Hospitali ya
Uhuru umefikia asilimia 92 na kazi zilizofanyika ni kusafisha eneo la
mradi,kuchimba na kujenga msingi, kujenga “frame” ya jengo pamoja na kuta,
kupiga “plaster” kuta pamoja na” skimming”, kuweka njia za mifumo ya
umeme,kupaua na kufunga gypsum board,kuchimba mashimo ya maji taka na kuweka
“rough floor” kwa ajili ya kuweka vigae
0 Comments