📌HAMIDA RAMADHANI
IMEBAINISHWA kuwa watu milion 1.35 hupoteza maisha kwa ajali za barabarani barani Afrika licha ya kuwa na magari kwa asilimia 2.
Akizungumza Jijini hapa katika maadhimisho ya kumbukumbu ya wahanga wa ajali za barabarani hapa nchini , Mwenyekiti wa Chama Cha Wanasheria kanda ya Dodoma (TLS) Mary Mushi amesema ajali za barabarani zina gharimu maisha ya watu hususani katika nchi za Afrika.
‘’Takwimu zinaonesha kuwa Nchi za Afrika zinaongoza kwa kuwa na ajali nyingi za barabarani Duniani kuliko nchi zilizopo katika mabara mengine, na Afrika ina magari asilimia 2 tu Duani’’, alisema Mushi.
Aidha Mushi amesema takwimu zinaonesha kuwa watu Millioni 1.35 ufariki Dunia kila mwaka Afrika kutokana na ajali za barabarani hivyo hawanabudi kupinga na kuzuiaajali kwani inaathili Uchumi wa nchi.
Chama Cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) imeandaa kumbukumbu hii ili kupinga ajali za barabrani ikiwa pamoja na kutoa elimu kwa Wananchi jinsi ya kuzuia na atahari za ajali hizoMarry Mushi.
Mushia alitoa wito kwa Serikali ili kupunguza ajali za barabarani ifanye marekebisho ya Sheria ya 1973 katika kiwango cha ulevi anachotakiwakuwa nacho dereva na masharti ya mwendokasi.
Hata hivyo Mushi amesema anaamini Bunge lijalo linaweza kufanya marekebisho ya sheria kwani walishapeleka mapendekezo ya marekebisho ya sheria Serikalini.
Naye Mkuu wa kikosi cha Usalama Barabarani Dodoma SP Prakson Rugazia amesema kuwa, kwa upande wa Tanzania vizibiti mwendo vimesaidia sana kupunguza ajali za barabarani.
Hivi sasa ajali za barabarani hapa Tanzania zimepungua sana n ahii ni kutokana na vizibiti mwendo ambavyo vimefungwa katika mabasi ya abiria na baadhi ya magariSP Rugazia.
Mkuu huyo amesema mbali na vizibiti mwendo hivyo lakini baadhi ya adhabu zimeongezeka pamoja na elimu inayotolewa na jeshi hilo kupitia vyombo vya habari,makanisani,misikitini na kwenye vijiwe vya bodaboda.
Aidha SP Rugazia amesema ajali hizo hizo zinasababishwa mapungufu ambayo yanatokanana makosa ya kibinadamu ambayo yapo kwa asilimia 6,ubovu wa vyombo vya usafiri asilimia 16 na hali ya ubovu wa miundombinu asilimia 8.
Hata hiyvo SP Rugazia
amesema kwa sasa watu wanatengeneza magari yao hakuna magari mabovu barabarani
hali inayochangia pia kupunguza ajali za barabarani.
0 Comments