WADAU WA SEKTA YA AFYA WATAKIWA KUTOA HUDUMA BORA



📌HAMIDA RAMADHANI

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Afya Maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto,Profesa Mabula Nchemba amewataka wadau wa Sekta ya  Afya Nchini   kutoa huduma bora  za afya kwa jamii zinazo endana na Uchumi wa Kati.

Aidha Katibu Mkuu huyo amesema Uchumi wa Kati lazima uendane na miundo mbinu Bora ya Majengo ,Vifaa tuna vya kisasa na utoaji huduma ulio Bora.

Hayo yamesemwa jana Jijini hapa na  Prof.Nchemba wakati akifungua kongamano la Saba la  wadau wa Afya (Tanzania Health Summit) lililofanyika katika Ukumbi wa St. Gaspar pembezoni kidogo mwa Jiji la Dodoma.

Niwatake wadau wa Afya nendeni mkatoe huduma katika jamii zenye kiwango kinachoendana na Uchumi wa Kati, kuanzia matibabu hadi miundombinu.
Prof.Nchemba

Prof. Nchemba  amesema watanzania wa hali ya chini,wamekuwa wakifanya shughuli zinazoipatia serikali kodi,lakini wamekuwa wakipata changamoto kubwa katika upatikanaji wa huduma za afya.

Aidha Prof Nchemba amesema katika kuhakikisha kwamba wananchi wa kipato cha chini wanapata matibabu yanayoendana na uchumi wa kati,ni lazima tujadili jinsi gani mwananchi huyo anaweza kupata huduma nzuri bila gharama kubwa.

"Mkulima aliyechangia kodi kwa kilimo akihitaji kwenda kupata matibabu anatakiwa kutibiwa kwa gharama nafuu ambayo hatoshindwa kuimudu,"amesema Profesa Mchemba.

Katika kuhakikisha kwamba ilo linatekelezeka,serikali imetoa kipaumbele katika matibabu ya  magonjwa yasioambukiza kwa kuwa na madaktari bingwa wa magonjwa hayo.

Profesa Mchemba amesema pia serikali imejikita katika kuoungyza changamoto katika magonjwa yasioambukiza na yanayoambukiza akitolea mfano kwa watoto wadogo pamoja na wanawake.

"Serikali imetengeneza miundombinu ya kutosha lakini bado inaendelea na jitihada za kuhakikisha kwamba inaboresha sekta ya afya,hivyo wataalamu wetu mnatakiwa muwe na ujuzi wa kutosha ili kupata matokeo chanya katika sekta hiyo,"amesema Profesa Mchemba.

Naye rais Tanzania Health Summit Dkt.Omary  Chilo amesema watakayojadili katika kongamano hilo watayafikisha Serikalini ili yafanyiwe kazi kisera.

Dkt Chilo amesema watatumia mkutano huo kujadili masuala mbalimbali ya Afya pamoja na Changamoto zilizopo ambapo watatoa mapendekezo Serikali I ili  yakafanyiwe kazi.

Naye Mjumbe wa Bodi ya Tanzania  Health Summit Dkt. Ntuli Kapongwe kutoka Ofisi yabRais Serikali za Mitaa na Utawala Bora Tamisemia amesema kwa kiasi kikubwa Serikali imefanya maboresho katika kipindi kilichopita katika Sekta ya Afya.

Aidha Kapongwe amesema watahakikisha mapendekezo yatakayotolewa leo katika mkutano huo watahakikisha wanayapeleka sehemu husika kwaaji ya kufanyika kazi.

 

Post a Comment

0 Comments