📌HAMIDA RAMADHANI
JUMLA ya wadau 354 kutoka nyanja mbalimbali ya sekta ya Afya wanatarajia kushiriki kongamano la Afya Tanzania Health Summit linalotajia kufanyika Jijini Dodoma Novemba 25-26.
Akiongea na waandishi wa habari leo jijini hapa Rais wa kongamano la Afya Tanzania Health Summit Dkt. Omary Chillo amesema kongamano hilo ni la Saba kufanyika na lengo ni kujadili uchumi wa kati unavyoendana na nyanja ya Afya.
Dkt Chillo amesema katika kongamano hilo tasisi zisizo za Kiserikali zitatoa maada na kujadili ni jinsi gani hasa wataweza kuboresha afya ya Jamii kwa wananchi.
Aidha amesema katika mkutano huo watatoa mrejesho wa mikutano mingine iliyowahi kufanyika na kutoa mapendekezo ya Nini hasa kifanyike katika kuboresha sekta ya afya kipindi hiki Cha uchumi wa Kati.
Malengo makuu ya kongamano hili ni kubadilisha uzoefu na kuona tunafanyaje kazi hasa kipindi hikitulichoingia uchumi wa Kati katika taifa letu pendwa la Tanzania.Dkt Chillo.
Na kuongeza kusema kuwa "Kutakuwepo na maonyesho mbalimbali ya masuala ya afya na wabunifu watako shiriki katika kongamano hilo watapatiwa zawadi," amesema
Pia ametoa wito kwa Watu ambao bado hawajajiandikisha ili na washiliki pamoja katika kongamano hilo ili kuleta chachu katika sekta ya afya na kuboresha mifumo ya afya zaidi nchini
Hata hivyo katika
kongamano hilo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya Prof
Magula Mchembe na atakayefunga kongamano hilo ni Katibu Mkuu ofisi ya Raid
Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Muhandisi Joseph
Nyamhanga
0 Comments