📌NA BEN BAGO
UCHAGUZI wa Rais,Makamu wa Rais na Wajumbe wa Bodi ya Muungano wa Vialbu vya
Habri nchini (UTPC) umekamilika hii leo mjini Morogoro.
Katika uchaguzi huo Deogratius Nsokolo ambaye ni Mwenyekiti wa Klabu ya
Waandishi wa Habari Mkoa wa Kigoma ametetea nafasi yake kwa kupata ridhaa ya
wajumbe kuongoza taasisi hiyo kwa awamu ya pili.
Deo Nsokolo akipiga kura |
Nsokolo amepata kura 72 katika kura
83 ziliopigwa na wajumbe 83 huku mpinzani wake Edwin Soko ambaye ni Mwenyekiti
wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza akipata kura 11 pekee.
Matokeo hayo yanampa nafasi Deogratius Nsokolo kutumikia nafasi ya Urais wa
UTPC kwa miaka mingine mitano kuanzia 2020-2025 ambapo awali alitumika katika
nafasi hiyo mwaka 2015-2020.
MAKAMU WA RAIS
Pendo Mwakyembe akipiga kura yake |
Katika nafasi ya Makamu wa Rais,Pendo Mwakiembe (Katibu-Mara Press Club)
aliibuka na ushindi wa kura 65 na kumshinda mpinzani wake Lulu George
(Mwenyekiti-Tanga Press Club) aliyepata kura 18
UJUMBE WA BODI YA UTPC
Sambamba nafasi hizo za juu,mfumo wa bodi ya UTPC inaundwa pia na wajumbe
wengine 8 kwa uwino sawa wa jinsia.
WAGOMBEA WANAWAKE
Hadija Omar akipiga kura yake |
Walioshinda nafasi ya Ujumbe wa bodi ya UTPC ni;
1. Hadija Omar 48 (Mweka Hazina-Lindi Press Club)
2. Lilian Lucas 51(Katibu-Morogoro Press Club)
3. Salma Abdul 62 (Mweka Hazina-Tabora Press Club)
4. Paulina David 63 (Mweka Hazina-Mwanza Press Club)
Jumla ya kura zilizopigwa ni 83
WAGOMBEA WANAUME
Frank Leonard akipiga kura yake |
Walioshinda Ujumbe wa Bodi ni;
1. Mussa Yusuf 51 (Mwenyekiti-Central Press Club Dodoma)
2. Cloud Gwandu 61(Mwenyekiti Arusha Press Club)
3. Frank Leonard 64 (Mwenyekiti Iringa Press Club)
4. Abdallah Mfaume 69 (Zanzibar)
Kura zilizopigwa ni 83
Pia Bodi hiyo inaundwa na Mjumbe Mtaalamu Mshauri wa Masuala ya fedha ambapo
mgombea alikuwa mmoja tu Bw. Eliazer Mafuru na akazoa kura zote 83 za ndiyo
0 Comments