📌NA AMIDA RAMADHAN
MFUMUKO wa bei wa
Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Oktoba ,2020 umebaki kuwa asilimia 3.1kama
ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia mwezi Septemba,2020..
Hayo yamebainishwa Leo jijini hapa na Kaimu Mkurugenzi wa Sensa ya watu na Takwimu za Jamii,Ruth Minja wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini.
Amesema kuwa Mfumuko wa Bei kwa mwaka ulioishia mwezi Oktoba ,2020 kuwa sawa na mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Septemba 2020 ambapo umechangiwa kupungua na kuongezeka kwa bei za bidhaa ya bidhaa za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula kwa kipindi kilichoishia mwezi Oktoba ,2020 zikilinganishwa na bei za mwezi Oktoba ,2019.
Akibainisha baadhi ya bidhaa za vyakula zilizopungua bei kwa mwezi Oktoba,2020 zikilinganishwa na bei za mwezi Oktoba ,2019 kuwa ni mchele kwa asilimia 4.2, mahindi kwa asilimia 12.4, unga wa mahindi kwa asilimia 3.2,unga wa ngano kwa asilimia 0.9 ,unga wa mtama kwa asilimia 0.8 ,unga wa muhogo kwa asilimia 1.4, mihogo mibichi kwa asilimia 2.5, viazi vitamu kwa asilimia 5.4 na ndizi za kupika kwa asilimia 6.3.
Aidha emefafanua kuwa kwa upande mwingine baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula zilizoongezeka bei kwa mwezi Oktoba ,2020 zikilinganishwa na bei za mwezi Oktoba ,2019 ni pamoja na mavazi kwa asilimia 2.2, gesi ya kupikia kwa asilimia 6.5, mkaa kwa asilimia 8.8, ukarabati wa vifaa vya usafiri kama magari kwa asilimia 8.3 na samani kwa asilimia 1.4 .
Katika hatua nyingine akiongelea hali ya mfumuko wa bei kwa nchi za Afrika Mashariki kwa mwaka ulioishia mwezi Oktoba 2020 kwa upande wa nchini Kenya mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Oktoba 2020 umeongezeka hadi asilimia 4.84 kutoka asilimia 4.20 kwa mwaka ulioishia mwezi Septemba 2020.
Hata hivyo kwa upande wa Uganda
mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Oktoba ,2020 umebaki kuwa asilimia 4.5
kama ilivyo kuwa kwa mwaka ulioishia mwezi Septemba ,2020.
0 Comments