RED CROSS KUHAKIKISHA WANAFIKA KILA KIKIJI



NA HAMIDA RAMADHANI

RAIS wa Taasisi ya  Msalaba Mwekundu Nchini (Red Cross)David Mwakiposa amesema angependa kuona katika Kijiji kunakuwepo na huduma  ya Msalaba Mwekundu.

Aidha amesema Red Cross inatoa huduma mbalimbali katika jamii siyo kuchangia damu tu.

Mwakiposa ameongea hayo Jana Jijini hapa alipokuwa akizindua semina ya kuwajengea vijana wa Redcross uwezo katika kukabiliana na majanga mbalimbali ya kusaidia jamii.a

Unajua Kuna watu wanafikiri Red Cross kazi yao ni kuchangia damu tu!! Siyo kweli ,Taasisi hii inafanya Mambo mengi Sana katika jamii,lengo likiwa ni kutoa msaada kwa watu waliopata majanga mbalimbali.

Aidha Mwakiposa alisema mkakati wao ni kuongeza nguvu za Kiuchumi  katika Taasisi hiyo ili Tanzania iwe mahali salama pa kuishi .

Naye Katibu Mkuu wa Red Cross Tanzania Julius Kejo amesema lengo la Taasisi hiyo ni kuongeza vijana wengi watakaokuwa wakitoa huduma mbalimbali katika jamii.

Lengo letu ni kuingiza vijana wengi ili kupata rasimali watu ya kutosha, ambao pia tunawaandaa kuwa viongozi wa kesho

Julius Kejo

Mtendaji Baraza la Vilana Red Cross Tanzania Nobert Vyagusa alisema kuwa semina hiyo imejumuisha makatibu na vijana kutoka Tanzania nzima,ili kuwapa uwezo katika shughuri zao wanazofanya.

Lengo la semina hiyo ni kuwajengea uwezo kiutendaji vijana,lakini pia kuwafahamisha vijana wawe mabalozi wazuri katika jamii

Norbet Vyagusa.

Post a Comment

0 Comments