📌MWANDISHI WETU, KAGERA
Rais wa Muungano wa klabu za Waandishi wa habari
Tanzania UTPC Deogratius Nsokolo, amekutana na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia
Generali Marco Gaguti na kuzungumzia ushirikiano baina ya Serikali na Kagera
Press Club.
Brigedia Generali Gaguti amesema ofisi yake
itaendelea kutoa ushirikiano wa dhati kwa waandishi wa habari kutokana na
umuhimu wa taaluma hiyo katika kusaidia maendeleo ya mkoa.
Waandishi ni muhimu sana, napenda tushirikiane na tuelezane juu ya kila kitu na pale inapotokea changamoto basi tuipatie ufumbuzi kwa pamoja.
Brigedia Generali Gaguti
Amesema yapo mambo mengi ya maendeleo ambayo
yamefanyika na yanaendelea kufanyika katika Mkoa hivyo ni jukumu la waandishi
kueleza juu ya changamoto na mafanikio.
Rais wa Muungano wa Klabu
za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) Deogratius Nsokolo
( kulia) akiwa
na na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Generali Marco Gaguti (kushoto)
baada ya kutembelea ofisini kwake.
Kwa upande wake Rais wa UTPC amesema kwa sasa
waandishi katika kila mkoa wanawajibu wa kuimarisha uhusiano na Serikali na
wadau wengine bila ya kuathiri utendaji wao wa kazi na kuisaidia jamii kwa
kufichua maovu na kutoa habari ambazo zitasaidia watawala kutenda mema kwa
wananchi.
Aidha amemuomba mkuu wa mkoa kuanzisha utaratibu wa
kukutana na waandishi wa habari walau mara moja kila mwaka ili kubadilishana
mawazo lakini pia kupata fursa ya kujibu maswali mbalimbali toka kwa waandishi,
ombi ambalo amelikubali.
0 Comments