MWENYEKITI ATAKA MAKUNDI YA UCHAGUZI YAVUNJWE

 


📌BARNABAS KISENGI

MWENYEKITI wa Mtaa wa Chinyoyo Kata ya Kilimani jijini Dodoma Faustina Bendera amewataka wananchi wa mtaa huo kuvunja makundi ya kisiasa ambayo walikuwa nayo katika kampeni za Uchaguzi uliofanyika mwezi Oktoba mwaka huu.

Kauli hiyo ameitoa wakati kuzungumza na mwandishi wa habari wa blogu hii wakati akielezea mafanikio ya mtaa huo kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita (2015 hadi 2020) katika mtaa huo na kuwataka wakazi wa mtaa huo kuchapa kazi ili kujiletea maendeleo zaidi. 

 Bendera amesema kazi iliyobaki kwa sasa ndani mtaa huo ni moja tu ya kusukuma maendeleo ya wakazi wa mtaa huo.

Katika kipindi cha kampeni za uchaguzi tuligawanyika kutokana na itikadi za vyama,uchaguzi umepita  hivyo nawasihi wananchi wa mtaa huu kuvunja makundi na kuungana kwa pamoja na viongozi waliochaguliwa kwenye sanduku la kura kuleta maendeleo.

Faustina Bendera.

Kiongozi huyo wa mtaa amesema katika kipindi cha miaka mitano iliyopita anajivunia kuleta baadhi ya mafanikio ikiwemo zoezi la upimaji wa ardhi kwa kufanya maboresho kwa mtaa wangu ambao tangu tupate uhuru ulikuwa haujapimwa wananchi walikuwa wakilishi hawajui hatima yao.

Kwa kushirikiana na viongozi wa ngazi mbalimbali na kamati ya makazi ya mtaa na ofisi ya Mkurugenzi kwa pamoja tumefanikisha ndoto ya muda mrefu, sasa wananchi wanalala kwa amani na wanaweza kupata mikopo kwenye taasisi za kifedha baada ya kupimiwa ardhi katika maeneo yao na kuweza kujenga nyumba za kisasa zinazoendana na jiji la Dodoma.

Bendera amesema kutokana na  Kata ya Kilimani kutokuwa na eneo la huduma za kijamii ,serikali ya mtaa huo imetenga eneo la kujenga shule ya msingi sekondari ya Kata, zahanati, soko,stendi na kituo cha Polisi cha Kata.

Post a Comment

0 Comments